Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Taarifa Kwa Umma Kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI:Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Mb) amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Bw. Dennis. N. Mrema

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene  -- JAMHURI YA MUUNAGANO YA TANZANIA   Ofisi ya Rais-TAMISEM...


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene 
--
JAMHURI YA MUUNAGANO YA TANZANIA
  Ofisi ya Rais-TAMISEMI,
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Mb) amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Bw. Dennis. N. Mrema kuanzia leo tarehe 07 Januari, 2016 kwa kosa la kusababisha upotevu wa Mapato ya Serikali kutokana na urasimu wa kukusudia, mazingira ya rushwa na uzembe katika utoaji wa leseni za Biashara.

Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ameelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala na nafasi yake kukaimiwa na mtu mwingine ili kupisha uchunguzi zaidi juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake.

Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI amefikia uamuzi huu baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa Wafanyabiashara ambao wamemlalamikia Mtendaji huyu kwa ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za utoaji wa Leseni za Biashara, Urasimu na Mazingira ya rushwa.

Katika uchunguzi wa awali uliofanyika kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Ilala mambo yafuatayo yamegundulika:
  •  Ukiukwaji wa Makusudi wa Sheria,  Kanuni  na Taratibu  za utoaji wa Leseni za Biashara.
  •  
  • Kutoa Leseni za Biashara zaidi ya 843 bila kuwa na Vyeti vya uthibitisho wa Walipa kodi ‘Tax Clearance Certificates” hivyo kuikosesha Serikali Kodi ya Mapato.
  • Kukaa na fomu za Wafanyabiashara 336 kwa muda mrefu bila sababu za msingi.
  •  Kukiuka Mwongozo wa Mkataba wa Huduma kwa wateja ambao unamtaka Afisa Biashara kutoa Leseni za Biashara ndani ya siku 2 hadi 3 baada ya muombaji kuwasilisha maombi yake ya kupatiwa Leseni ya Biashara.
Aidha, Mheshimiwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais-TAMISEMI amewaagiza Maafisa Biashara wote nchini watoe huduma za Leseni kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu , kuacha urasimu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Imetolewa na:
   Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini
   Ofisi ya Rais-TAMISEMI,
   07 Januari, 2016.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Taarifa Kwa Umma Kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI:Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Mb) amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Bw. Dennis. N. Mrema
Taarifa Kwa Umma Kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI:Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Mb) amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Bw. Dennis. N. Mrema
http://3.bp.blogspot.com/-9h50g0K9SBo/Vo55fY2hy8I/AAAAAAADdcI/P4WCmCNQlp4/s640/Hotmix%2B1102a.JPG
http://3.bp.blogspot.com/-9h50g0K9SBo/Vo55fY2hy8I/AAAAAAADdcI/P4WCmCNQlp4/s72-c/Hotmix%2B1102a.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/taarifa-kwa-umma-kutoka-ofisi-ya-rais.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/taarifa-kwa-umma-kutoka-ofisi-ya-rais.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago