Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

SOMA KWA MAKINI RATIBA YA MKUTANO WA WABUNGE WOTE PAMOJA NA VIKAO VYA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE TAREHE 20 JANUARI – 25 JANUARI, 2016

Ofisi ya Bunge inapenda kuwafahamisha Waheshimiwa Wabunge na Wananchi kwa ujumla kuwa, uteuzi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bung...Ofisi ya Bunge inapenda kuwafahamisha Waheshimiwa Wabunge na Wananchi kwa ujumla kuwa, uteuzi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge utafanyika kesho Alhamisi tarehe 21 Januari, 2016, na kufuatiwa na Uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati husika pamoja na Kamati kupatiwa maelezo juu ya Wajibu, kazi na Mipaka ya kazi ya Kamati na kupokea na kujadili Mpango kazi wa Kamati unaoishia Juni, 2016.Kwa kuzingatia Kanuni ya 111 ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013 siku ya Ijumaa tarehe 22 hadi Jumamosi tarehe 23 Januari kutakuwa na Mkutano wa Wabunge wote ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na lengo la kuwafahamisha Wabunge kuhusu Kanuni za Kudumu za Bunge na Uendeshaji wa Bunge, Nadharia ya mgawanyo wa Madaraka katika Mihimili ya Dola, Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Mambo Mengine ya Kiserikali.Aidha, Kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi ambacho wajumbe wake ni Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge chini ya Uenyekiti wa Mhe. Spika, kinatarajiwa kufanyika Siku ya Jumapili tarehe 24 Januari, 2016, ambapo Jumatatu tarehe 25 Januari, 2016 itakuwa ni siku mahususi kwa Wabunge kupata maelezo kuhusu Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano.Ratiba ya Shughuli za Mkutano wa pili wa Bunge unaotarajiwa kuanza Jumanne tarehe 26 Januari, 2016 itatolewa baadae.Imetolewa na,

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano.

Ofisi ya Bunge,

S.L.P 9133,

DAR ES SALAAM

20 Januari, 2016.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: SOMA KWA MAKINI RATIBA YA MKUTANO WA WABUNGE WOTE PAMOJA NA VIKAO VYA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE TAREHE 20 JANUARI – 25 JANUARI, 2016
SOMA KWA MAKINI RATIBA YA MKUTANO WA WABUNGE WOTE PAMOJA NA VIKAO VYA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE TAREHE 20 JANUARI – 25 JANUARI, 2016
http://3.bp.blogspot.com/-yaij4wXDMJM/Vp-T5D84ohI/AAAAAAADd3k/ukM2auOL46s/s320/Screen%2BShot%2B2016-01-20%2Bat%2B4.46.05%2BPM.png
http://3.bp.blogspot.com/-yaij4wXDMJM/Vp-T5D84ohI/AAAAAAADd3k/ukM2auOL46s/s72-c/Screen%2BShot%2B2016-01-20%2Bat%2B4.46.05%2BPM.png
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/soma-kwa-makini-ratiba-ya-mkutano-wa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/soma-kwa-makini-ratiba-ya-mkutano-wa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago