Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU MISAADA ILIYOKATALIWA, KATIBU MKU AKABIDHIWA OFISI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari kuh...

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu watumishi wa wizara hiyo nchini kote kupokea misaada inayotolewa na taasisi mbalimbali na watu wenye moyo wa kusaidia jamii  bila kujali itikadi za siasa au dini isipokuwa wahakikishe misaada hiyo inakidhi viwango vinavyotakiwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akikabidhiwa nyaaraka muhimu na aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Donan Mmbando.
--
Na Magreth Kinabo –Maelezo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema misaada inayotolewa na watu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia jamii ni lazima iwe imekidhi viwango vya ubora, hivyo haitakiwi kuangaliwa kwa vigezo vya dini, itikadi wala siasa.

 Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake baada kituo kimojwapo nchini kukataa misaada iliyotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare wa Chama cha Wananchi(CUF), hivi karibuni.

 Dkt. Ulisubisya  alisema hivi karibuni gazeti moja la kila siku la hapa nchini liliripoti kwamba misaada iliyotolewa na Mbunge huyo, katika baadhi vituo afya Zahanati  kwa ajili ya wajawazito  kukataliwa.

“Serikali ina sera ya kusaidia jamii hususan misaada inayotolewa  kwenye huduma za afya, ambayo inakidhi viwango vya ubora kulingana Sheria , kanuni na taratibu za Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA),” alisema Katibu Mkuu huyo.  

Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari kiliripoti kwamba baadhi ya wakuu wa vituo vya afya na zahanati katika Manispaa ya Bukoba, wamegoma kupokea misaada kwa ajili ya wajawazito uliotolewa na kwa madai ya kupewa maelekezo na Serikali.

Dkt. Ulisubisya aliwataka watendaji wa afya wa vituo hivyo kuwa wasiangalie misaada hiyo kwa misingi ya dini, itikadi na kisiasa.
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo aliwataka watu mbalimbali wenye lengo la kutoa misaada katika vituo vya afya kuhakikisha kwamba imekidhi viwango viliyowekwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
 Katika hatua nyingine aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando alikabidhi ofisi hiyo kwa Katibu Mkuu huyo mpya.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU MISAADA ILIYOKATALIWA, KATIBU MKU AKABIDHIWA OFISI
SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU MISAADA ILIYOKATALIWA, KATIBU MKU AKABIDHIWA OFISI
http://2.bp.blogspot.com/-WPoru_QKcdU/VovqoIojmuI/AAAAAAADdWo/chF9lCJvbQY/s640/111.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-WPoru_QKcdU/VovqoIojmuI/AAAAAAADdWo/chF9lCJvbQY/s72-c/111.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/serikali-yatoa-tamko-kuhusu-misaada.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/serikali-yatoa-tamko-kuhusu-misaada.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago