Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Rais Dr John Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma Maalim  ---- Na E...

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma Maalim 
----
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
 Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.

Vile vile Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha na kuwataka Mabalozi hao kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliyechini yao leo hii.
 
Mabalozi hao ni Bi Batilda Salha Buriani, aliyeko Tokyo, Japan, Dkt. James Alex Msekela, aliyeko Rome, Italia.
 
Kwa mujibu wa Balozi Sefue, Rais pia amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan Kallaghe ambaye anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa ambapo atakapopangiwa kazi nyingine.
 
Balozi Sefue alisema kuwa hadi sasa vituo vya Ubalozi ambavyo viko wazi ni London nchini Uingereza kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. Kallaghe, Brussels nchini Ubelgiji kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous Kamala kuchaguliwa kuwa Mbunge, Rome nchini Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex Msekela na Tokyo nchini Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda Buriani. 
 
Vituo vingine vya Ubalozi ambavyo viko wazi ni Kuala Lumpar nchini Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi Dkt. Aziz Ponray Mlima kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa na Brasilia nchini Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis Malambugi.
 
Wakati huo Balozi Sefue alisema kuwa Rais ametengua uteuzi wa Mhandisi Madeni Juma Kipande kabla hajathibitishwa kwenye cheo chaKatibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Rais Dr John Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait
Rais Dr John Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait
http://4.bp.blogspot.com/-X78QIVr6Aow/VqZLZ_SwVEI/AAAAAAADeJ8/zuAKuE5Dkmo/s640/DSC_0209.JPG
http://4.bp.blogspot.com/-X78QIVr6Aow/VqZLZ_SwVEI/AAAAAAADeJ8/zuAKuE5Dkmo/s72-c/DSC_0209.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/rais-dr-john-magufuli-amemteua.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/rais-dr-john-magufuli-amemteua.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago