Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

PICHA NA TAARIFA RASMI KUTOKA IKULU:RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Wilia...

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
---
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.Jaji Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.

"Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo" alisisitiza Jaji Warioba.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

07 Januari, 2016

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: PICHA NA TAARIFA RASMI KUTOKA IKULU:RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
PICHA NA TAARIFA RASMI KUTOKA IKULU:RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
http://2.bp.blogspot.com/-UoIAYkA9ohc/Vo6A0oAmx5I/AAAAAAADde8/cb1QDop0EXA/s640/2.JPG
http://2.bp.blogspot.com/-UoIAYkA9ohc/Vo6A0oAmx5I/AAAAAAADde8/cb1QDop0EXA/s72-c/2.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/pichaa-na-taarifa-rasmi-kutoka.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/pichaa-na-taarifa-rasmi-kutoka.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago