Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

PICHA KUTOKA IKULU:RAIS DR JOHN MAGUFULI ALISISIMUA JIJINI ARUSHA KWA MAVAZI YA KIJESHI NA HOTUBA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mbauda Mkoani Arusha hawaonekani ...

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mbauda Mkoani Arusha hawaonekani pichani wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo Medani.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma bango alilokabidhiwa na mwananchi mmoja katika eneo la Kona ya Nairobi Mkoani Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mianzini Mkoani Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha waliojitokeza kumsalimia wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo Medani.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Arusha katika eneo karibu na chuo cha Arusha Tech. Wananchi hao walifunga barabara ili wapate nafasi ya kumuona Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli
  Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani Arusha
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la Ufungaji.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo Medan.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati waufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akishuhudia matukio ya zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipewa maelezo ya zana mojawapo ya zana za Kivita katika Zoezi la Onesha Uwezo Medani Mkoani Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara baada ya kufunga zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.Picha na IKULU
---
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameonya kuwa wilaya ama Mkoa wowote ambao utakumbwa na njaa, itakua ni kipimo tosha cha kuonesha kuwa Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa wilaya husika hafai kuendelea na wadhifa huo.
 
Rais Magufuli ametoa onyo hilo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti aliposimamishwa na wananchi wa Arusha Mjini akiwa njiani kuelekea Monduli ambako amefunga  "Zoezi Onesha Uwezo Medani" lililoandaliwa na kutekelezwa na kamandi ya Jeshi la nchi kavu ambalo ni sehemu ya jeshi la wananchi wa Tanzania.

Amesema kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi, Viongozi wa Wilaya na Mikoa wana wajibu wa kuwahamasisha wananchi kuzalisha mazao ya chakula ili wasikumbwe na njaa.

Rais Magufuli ameendelea kuwasihi wananchi wa Arusha Mjini kuwa uchaguzi umekwisha na kwamba kilichobaki sasa ni kazi huku akiwahimiza kufanya kazi za uzalishaji mali ikiwemo kilimo.

"Naomba ndugu zangu mniombee, na ninapenda kuwahakikishia kuwa sitawaangusha. Yote niliyoahidi nitayatekeleza bila kubagua nawaombeni mnipe muda na muwe wavumilivu" alisisitiza Rais Magufuli.

Amerejea kauli zake alizozitoa jana alipoingia mkoani Arusha kuwa atendelea kuwashughulikia wezi, mafisadi na watendaji wote wa serikali ambao wamekua wakijineemesha kwa kufuja mali ya umma kupitia kampeni yake ya "Kutumbua Majipu" na amewaomba watanzania wote waendelee kumuombea ili atumbue majipu yote hadi yaishe.

 Rais Magufuli amelazimika kuzungumza na wananchi wa Arusha Mjini waliokuwa wamekusanyika kwa maelfu kando kando mwa barabara na hivyo kujikuta akisimamishwa na wananchi wa Sanawali, Tekniko, Ngarenaro, Kona Ya Nairobi, Mbauda, Majengo Na Kisongo.

Akiwa katika eneo la Ngarenaro wananchi wamelalamikia vitendo vya rushwa vilivyokithiri katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso na pia katika eneo la Kona ya Nairobi wananchi wamelalamikia kero za kelele na uchafu wa kiwanda kilichojengwa kandokando mwa barabara ambapo Rais Magufuli ameahidi kufanyia kazi kero hizo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha.
22 Januari, 2016

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: PICHA KUTOKA IKULU:RAIS DR JOHN MAGUFULI ALISISIMUA JIJINI ARUSHA KWA MAVAZI YA KIJESHI NA HOTUBA
PICHA KUTOKA IKULU:RAIS DR JOHN MAGUFULI ALISISIMUA JIJINI ARUSHA KWA MAVAZI YA KIJESHI NA HOTUBA
http://4.bp.blogspot.com/-xr6y5XNhLek/VqJZc8MT_nI/AAAAAAADeDQ/CObH8F4VX0I/s640/2.jpg
http://4.bp.blogspot.com/-xr6y5XNhLek/VqJZc8MT_nI/AAAAAAADeDQ/CObH8F4VX0I/s72-c/2.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/picha-kutoka-ikulurais-dr-john-magufuli_22.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/picha-kutoka-ikulurais-dr-john-magufuli_22.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago