Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MUKHTASARI WA HOTUBA YA BALOZI WA USWISI TANZANIA, BI. FLORENCE TINGUELY MATTLI, KATIKA UZINDUZI WA GLOBAL COMPACT NETWORK TANZANIA - HYATT, DAR ES SALAAM, JANUARI 19, 2016

MUKHTASARI WA HOTUBA YA BALOZI WA USWISI TANZANIA, BI. FLORENCE TINGUELY MATTLI, KATIKA UZINDUZI WA GLOBAL COMPACT NETWORK TANZANIA ...


MUKHTASARI WA HOTUBA YA BALOZI WA USWISI TANZANIA, BI. FLORENCE TINGUELY MATTLI, KATIKA UZINDUZI WA GLOBAL COMPACT NETWORK TANZANIA
 --
HYATT, DAR ES SALAAM, JANUARI 19, 2016
 
Uswisi ni kama mlezi wa Global Compact kwasababu wazo lake lilizaliwa mwaka 2000 kwenye
 mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) mjini Davos. Uswisi imekuwa 
mshiriki na mwanachama wa muda mrefu wa UN Global Compact (UNGC) na huchangia fedha 
na ushauri kwenye Bodi ya Utendaji mjini New York. Katika ngazi ya kimataifa, tumeshiriki 
kikamilifu kutetea upanuzi wa UNGC nchi za kusini mwa Dunia hasa Afrika.
 
Ushiriki wetu unatokana na msingi na imani ya Waswisi kuwa: kukuwa kwa dhamira ya
 jumuiya ya wafanyabiashara katika kuheshimu sheria za ajira, haki za binadamu na mazingira,
 na kutokomeza ufisadi na rushwa kutaleta mafanikio kwa wote. Biashara zitaweza kuongeza
 faida na kuwa endelevu zaidi, serikali itafaidika kwa ukuaji wa uchumi na ongezeko la mapato,
 na jamii itafaidika kutokana na ajira, ongezeko la kipato na huduma bora.
 
 
Wakati wazo la kuanzisha Global Compact Network linaanza Tanzania, Uswizi ilikuwa mstari 
wa mbele kushiriki katika kutafsiri kanuni zake ili ziweze kutumika na wafanyabiashara hapa
 nchini. Tukio la leo ni kilele cha mchakato huu na inaridhisha kuona kwamba jitihada zimeanza kuzaa matunda na bila shaka huu ni mwanzo tu.
 Serikali mpya imeahidi kuwa itaboresha mazingira ya biashara na inatarajia kuona ongezeko
 la mapato kwa kushirikiana na sekta binafsi. Rushwa imeonekana kwenye ripoti nyingi kama
 kikwazo kikubwa kwa maendeleo nchini Tanzania. Kupambana na rushwa ni sehemu ya 
kanuni za Global Compact na kwasababu Serikali pia imeipa kipaumbele mapambano haya,
 huu ni wakati sahihi kwa wote kuchukua hatua za pamoja katika suala hili muhimu.
 
Kanuni za Global Compacat zina manufaa katika kuongoza serikali na sekta binafsi kuelekea kwenye utawala bora wa mazingira ya biashara ambayo unaruhusu ushindani wa haki, biashara endelevu, na ukuaji wa uchumi utakaofaidisha wananchi wengi zaidi kupitia ajira na huduma bora. Tunaweza kusema kwa uhakika wadau wa maendeleo wanaunga ajenda hii.
 Mafanikio yatatokana na jitihada za viongozi wa biashara hapa Tanzania. Hivyo tunataka
 kuwapongeza wadau waliokuwepo tokea kuanza kwa Global Compact kwa mafanikio
 waliyopata hadi sasa. Tunataka kusisitiza kwamba sisi na wadau wengine wa kimataifa 
tuko sambamba na nyie lakini ni wafanyabiashara wenyewe wenye kuweza kuleta mabadiliko
 ya kudumu.
 

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MUKHTASARI WA HOTUBA YA BALOZI WA USWISI TANZANIA, BI. FLORENCE TINGUELY MATTLI, KATIKA UZINDUZI WA GLOBAL COMPACT NETWORK TANZANIA - HYATT, DAR ES SALAAM, JANUARI 19, 2016
MUKHTASARI WA HOTUBA YA BALOZI WA USWISI TANZANIA, BI. FLORENCE TINGUELY MATTLI, KATIKA UZINDUZI WA GLOBAL COMPACT NETWORK TANZANIA - HYATT, DAR ES SALAAM, JANUARI 19, 2016
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/mukhtasari-wa-hotuba-ya-balozi-wa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/mukhtasari-wa-hotuba-ya-balozi-wa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago