Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MAONESHO YA BIASHARA YA ESTHER LAND SHOW AFRIKA KUSINI YAVUTIA WAFANYABIASHARA WENGI ZAIDI KUTOKA TANZANIA

Na EmanuelMadafa,Mbeya,Mbeya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Afrika kusini   ( Esther Land Show ) ambayo hufanyika kila mwaka nc...


Na EmanuelMadafa,Mbeya,Mbeya
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Afrika kusini  (Esther Land Show) ambayo hufanyika kila mwaka nchini humo yameendelea kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi kutoka nchini Tanzania.

Pia Maonesho hayo hufanyika  katika mji wa Johnsburg ambapo kwa mwaka huu yanatalaji kuanzia Mwezi Machi  23 hadi  April 03 mwaka huu huku idadi ya wafanyabiasahara hao waliojitokeza imetajwa kufikia  zaidi ya watu  100 ,hasa kutoka  katika mikoa ya Kanda ya Ntanda za juu kusini.

Katika kufanikisha safari ya wafanyabiashara hao  kampuni ya  Blue  Bird Buleau De Change iliyopo Jijini Mbeya imeamua kudhamini safari hiyo kwa kutoa usafiri wa kwenda na kurudi kwa basi  la Twiga Intarnational  ambapo kila mfanyabiashara atachangia kiasi cha shilingi laki nne na nusu  (450000).

Akizungumza jijini mbeya, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Jankey Ndingo, amesema ziara hiyo imelenga kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na nchi ya Afrika ya kusini katika kujengeana uwezo ikiwa na kutangaza fursa zilizomo kwenye maeneo yao.
“Mji wa Johnsburg umekuwa ukiendesha maonesho ya biashara kila mwaka katika Sikukuu ya Pasaka, hivyo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakihudhuria maonesho haya lakini kwa mwaka huu tunataka kuwashirikisha wafanyabiashara wadogo ili nao wafike na kunufaika na fursa hiyo,”alisema.
  
Amesema, maonesho hayo yamejikita zaidi katika masuala ya matumizi ya mitambo mbalimbali kama vile mitambo ya kilimo,vifungashio pamoja na ile inayozalisha bidhaa zikiwa na kiwango cha ubora unaoendana na soko la kimataifa.

Amesema, Afrika kusini kumekuwa na soko kubwa la bidhaa za kitamudi na zao la tangawizi zinazozalishwa Tanzania hivyo ni vema wafanyabiashara wakatumia fursa hiyo kwenda kutafuta masoko na kuanza kusafirisha bidhaa hizo.

“kinachotakiwa kufanywa na wazalishaji ni kuhakikisha bidhaa zote zinakidhi kiwango cha ubora wa kimataifa,”alisema.

Aidha, amesema kuwa ziara hiyo inashirikisha wafanyabiashara wote wanaonesha nia ya kutaka kujifunza na kubadilika ili kuondoka na hali ya umaskini na kwamba safari hiyo itaanzia Mjini Mbeya kwa usafiri wa basi  kupitia njia ya Zambia na kwa gharama nafuu.Hata hivyo, amesema kuwa safari hiyo itakuwa ni ya kitalii zaidi kwani wafanyabiashara watapata fursa ya kutembelea maporomoko ya mto Zambezi yajulikanayo kama Victoria yaliyopo nchini Zambia na kwamba ziara hiyo itakuwa ya siku 13.

Mwisho.
Jamiimojablog

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MAONESHO YA BIASHARA YA ESTHER LAND SHOW AFRIKA KUSINI YAVUTIA WAFANYABIASHARA WENGI ZAIDI KUTOKA TANZANIA
MAONESHO YA BIASHARA YA ESTHER LAND SHOW AFRIKA KUSINI YAVUTIA WAFANYABIASHARA WENGI ZAIDI KUTOKA TANZANIA
http://2.bp.blogspot.com/-X1WaTBcBvRA/VqHZPOsWR6I/AAAAAAAAVkU/X_8cWP55wyA/s640/biz.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-X1WaTBcBvRA/VqHZPOsWR6I/AAAAAAAAVkU/X_8cWP55wyA/s72-c/biz.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/maonesho-ya-biashara-ya-esther-land.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/maonesho-ya-biashara-ya-esther-land.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago