Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

IKULU:RAIS DR JOHN MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA WAHITIMU CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI

  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Nch...


 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati alipowasili  katika chuo cha Maafisa wa Kijeshi Monduli Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi kwa cheo cha Luteni Usu, anayetazama katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paulo Peter Massao. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa jeshi kwa cheo cha Luteni Usu.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi katika viwanja vya Chuo hicho.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia gwaride lililokuwa likipita mbele yake  kutoa heshima.
 Gwaride la Wahitimu likipita kutoa heshima mbele ya mgeni rasmi  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli .
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Meja Generali Paulo Peter Massao. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi aliyefanya vizuri  O/Cdt. Mmang’anda katika Mafunzo hayo. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wapya hawapo pichani .
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma jarida  la Ngome baada ya kukamilika zoezi la kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wapya aliowatunuku Kamisheni pamoja na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Wananchi. 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na watoto waliofika kushuhudia tukio hilo la kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wapya wa Jeshi. Picha na IKULU
----
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Januari, 2016 ametunuku kamisheni kwa Maafisa wapya 205 wa jeshi la wananchi kundi la 57/15 katika Chuo cha mafunzo ya kijeshi (TMA) Monduli Mkoani Arusha.

Maafisa hao wapya wametunukiwa cheo cha Luteni Usu, ambapo kati yao 16 ni maafisa wanawake, na 189 ni maafisa wanaume.

Aidha, miongoni mwa maafisa wapya 205 waliotunukiwa kamisheni, maafisa 10 wametoka majeshi rafiki kutoka nchi za Uganda, Kenya na Burundi.Akiwa katika uwanja wa paredi wa chuo hicho Rais Magufuli amepokea heshima zote za kijeshi ikiwemo kupigiwa wimbo wa Taifa na kukagua gwaride rasmi lililojumuisha maafisa hao wapya.
Baada ya kutunukiwa kamisheni, Maafisa wapya wa jeshi wamekula kiapo na wametoa heshima kwa gwaride lililopita mbele ya Rais kwa mwendo wa pole na mwendo wa haraka.

Viongozi wengine waliokuwepo katika tukio hilo ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, Maafisa wa ngazi za juu jeshini na Maafisa wastaafu, viongozi wa mkoa na wilaya na wakufunzi kutoka nje ya nchi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kutoa kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la wananchi tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwezi Oktoba Mwaka jana.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha.
23 Januari, 2016.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: IKULU:RAIS DR JOHN MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA WAHITIMU CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI
IKULU:RAIS DR JOHN MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA WAHITIMU CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI
http://4.bp.blogspot.com/-tU0bJPkUG4c/VqO6_Ic7h9I/AAAAAAAIULA/GvcFaDPpwgo/s640/1%2B%25281%2529.JPG
http://4.bp.blogspot.com/-tU0bJPkUG4c/VqO6_Ic7h9I/AAAAAAAIULA/GvcFaDPpwgo/s72-c/1%2B%25281%2529.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/ikulurais-magufuli-atunuku-kamisheni.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/ikulurais-magufuli-atunuku-kamisheni.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago