Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema kuwa inaendelea kuboresha huduma za afya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kupitia utaratibu mpya wa madaktari Bingwa kuwaona wagonjwa kupitia Kliniki zilizoanzishwa katika hospitali hiyo.

  Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi Neema Mwangomo akizungumza leo jijini Dar es salaam  wakati wa mkutano na Vyombo vya...

 Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi Neema Mwangomo akizungumza leo jijini Dar es salaam  wakati wa mkutano na Vyombo vya habari amabapo aliwataka Watanzania kutumia huduma zinazotolewa na Hospitali hiyo ya Taifa  kwa kuwa inao wataalamu wakutosha kutimiza jukumu hilo la kuwahudumia wananchi.
 Mkuu wa Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa nje toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari leo jijini Dara es salaam  kuhusu utaratibu mpya wa utoaji wa Huduma kwa wagonjwa wa nje ambapo huduma zitakuwa zikitolewa kuanzia Jumatatu hadi jumamosi ikiwa ni moja ya mikakati ya Hosipitali hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi.
Mkuu wa Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa nje toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano ulioenga kueleza mikakati ya Hosipitai hiyo katika kuboresha huduma zake kwa wananchi.kushoto ni Afisa Uhusiano wa Hospitali hiyo Bi Neema Mwangomo na kushoto ni Muuguzi wa Hospitali hiyo Bi June Samwel. 
---
Na. Jovina Bujulu –MAELEZO.
Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema kuwa inaendelea kuboresha huduma za afya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kupitia utaratibu mpya  wa madaktari Bingwa kuwaona wagonjwa kupitia Kliniki zilizoanzishwa katika hospitali hiyo.

Mkuu wa Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa Nje wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam amesema kuwa utaratibu huo utawasaidia wagonjwa kupata huduma kwa wakati na kupunguza muda kusubiri huduma.

Amesema utaratibu huo utawahusu wagonjwa wote wanakwenda kutibiwa katika Hospitali ya Muhimbili na kuondoka hususan wale wanaolipa fedha taslimu na wale ambao ni wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bima za mbalimbali za Afya na watumishi ambao makampuni yao yana mikataba na Hospitali kutibu wafanyakazi wao.

Dkt. Mwenesano ameeleza kuwa tayari Kliniki hizo zimekwisha anza kufanya kazi na kuongeza kuwa katika hatua hiyo madaktari Bingwa pekee ndiyo watakaoona wagonjwa wakati wa siku za kazi kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni, pia jumamosi kuanzia saa 3 asubuhi hadi za 8 mchana.

“Muhimbili tumeamua kufanya mabadiliko haya kuanzisha Kliniki na kuwatumia  madaktari bingwa peke kwa lengo la kuboresha huduma zetu, awali tulikuwa na Kliniki hizi lakini huduma zake zilikuwa hazitolewi kwa kiwango cha kuridhisha kutokana na kutokuwepo kwa muda wa kutosha wa mdaktari hao kuhudumia wagonjwa” Amesisitiza.


Aidha, amefafanua kuwa wagonjwa wanaopatiwa rufaa kuja hospitali ya Muhimbili wataendelea na utaratibu wa kawaida wa kwenda na Barua  za Rufaa ili waweze kupatiwa huduma.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema kuwa inaendelea kuboresha huduma za afya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kupitia utaratibu mpya wa madaktari Bingwa kuwaona wagonjwa kupitia Kliniki zilizoanzishwa katika hospitali hiyo.
Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema kuwa inaendelea kuboresha huduma za afya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kupitia utaratibu mpya wa madaktari Bingwa kuwaona wagonjwa kupitia Kliniki zilizoanzishwa katika hospitali hiyo.
http://4.bp.blogspot.com/-3WNXqVVaygk/VqEQOLJuAEI/AAAAAAADd5w/_U7Zl0J2mhA/s640/2.JPG
http://4.bp.blogspot.com/-3WNXqVVaygk/VqEQOLJuAEI/AAAAAAADd5w/_U7Zl0J2mhA/s72-c/2.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/hospitali-ya-taifa-muhimbili-imesema.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/hospitali-ya-taifa-muhimbili-imesema.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago