Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

DAR, BAGAMOYO KUKOSA MAJI KWA SIKU MBILI

  SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwapo tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo y...


 

SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwapo tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini ya jiji la Dar es salaam, pamoja na baadhi ya maeneo  ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 48 kuanzia siku ya Jumamosi 23/01/2016 hadi Jumapili 24/01/2016.

Taarifa ya kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na kaimu meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi  Everlasting Lyaro, imeeleza kuwa sababu ya kuzimwa kwa mtambo huo, ni kuruhusu mkandarasi kuunganisha bomba jipya na bomba la zamani katika tanki la Maji wazo-Tegeta, zoezi ambalo linaashiria kukamilika kwa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini, hivyo kuondoa  tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini.

“Tunaelekea kwenye hatua za mwisho za kupokea Maji mengi kutoka mtambo wa Ruvu Chini baada ya kazi ya upanuzi inayoelekea kukamilika mapema mwezi February mwaka huu, na kiasi cha Maji kitaongezeka kutoka wastani wa Lita Milioni 182,000 zinazozalishwa sasa hadi Lita Milioni 270,000. Hivyo kuzimwa kwa mtambo huu ni moja ya hatua za mwisho-mwisho katika ukamilishaji wa Mradi wa Ruvu Chini” alisema Lyaro

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, DAWASCO imetoa wito kwa wateja na wananchi wote kuhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi muhimu ili kukidhi mahitaji husika kwa kipindi hicho chote.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa matengenezo hayo yatasababisha maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam kukosa Maji, pamoja na mji wa Bagamoyo vijiji vya Zinga, Kerege na Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani,  Mbezi Beach na Kawe.

Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili, Buguruni, Chang’ombe na KekoCOMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: DAR, BAGAMOYO KUKOSA MAJI KWA SIKU MBILI
DAR, BAGAMOYO KUKOSA MAJI KWA SIKU MBILI
http://1.bp.blogspot.com/-b1BZEv6_d54/Vp_YoX6q1CI/AAAAAAAAZYE/hrPjefRLU_0/s640/index.png
http://1.bp.blogspot.com/-b1BZEv6_d54/Vp_YoX6q1CI/AAAAAAAAZYE/hrPjefRLU_0/s72-c/index.png
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/dar-bagamoyo-kukosa-maji-kwa-siku-mbili.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/dar-bagamoyo-kukosa-maji-kwa-siku-mbili.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago