Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

AFYA YA ASKOFU KARDINALI PENGO YAZIDI KUIMARIKA.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Hospitali y...


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Hospitali ya Muhimbili mara baada ya kumtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Jenad Abdallah leo jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu, akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo, katika taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo,  Dk.Mpoki Ulisubisya na katikati ni  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto Dk. Godwin  Godfrey.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuitembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Jenabi Abdallah, Kulia ni Katibu wa Wizara hiyo, Dk.Mpoki Ulisubisya.
--

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKURUGENZI wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kiktwete ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Jenad Abdallah amesema kuwa afya ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo ina inaendelea vizuri tofauti na hali aliyokwenda nayo.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo alipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili Januari Mosi akisumbuliwa tatizo la moyo.

Amesema kuwa kutokana na huduma anayoipata katika taasisi hiyo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhadhama Polycap Kardinali Pengo hali yake ina imarika na si muda mrefu wanaweza kumruhusu.

Profesa Abdallah amesema hata kiongozi huyo akitaka kwenda nje kwa matibabu wataka kujiridhisha na huduma wanayoitoa.

Waziri wa Afya Maendeleo Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemtembelea Mhadhama Polycap Kardinali Pengo na kujioanea hali yake na kudai kuwa kiongozi huyo amemkuta akiwa amekaa na tofauti na baadhi mitandao ya Jamii si Globu ya Jamii ya Michuzi zikidai kuwa yuko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU).

Amesema huduma anayoipata Kardinali Pengo atakuwa Balozi mzuri wa kuelezea huduma ya taasisi ya moya ya Jakaya Kikwete na kuwataka watu wengine kwenda kupata huduma hiyo na sio kwenda nje.

Amesema Serikali itaendalea kuboresha huduma hiyo kwa sasa kwa viwango vya dunia Tanzania imefikia asilimia nne na kiwango cha kimataifa cha juu ni asilimia sita.

Wakati huu Waziri huyo amekutana na menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili kusikia changamoto zinazowakabili pamoja na mafanikio walioyapata.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: AFYA YA ASKOFU KARDINALI PENGO YAZIDI KUIMARIKA.
AFYA YA ASKOFU KARDINALI PENGO YAZIDI KUIMARIKA.
http://2.bp.blogspot.com/-POuLKN0LBwc/Vo5_GIFWXlI/AAAAAAADdeQ/9mLs0KfIAJA/s640/DSC_7106.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-POuLKN0LBwc/Vo5_GIFWXlI/AAAAAAADdeQ/9mLs0KfIAJA/s72-c/DSC_7106.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/afya-ya-askofu-kardinali-pengo-yazidi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/afya-ya-askofu-kardinali-pengo-yazidi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago