Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yatangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando akionyesha aina ya dawa zinazotakiwa...

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando akionyesha aina ya dawa zinazotakiwa kugawiwa kwa umma wakati alipotangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya Waandishi wa Habari  jana 17 Desemba, 2015.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya kutangazwa kwa Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyotolewa leo 17 Desemba, 2015 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Picha zote na Benedict Liwenga
-----
Na Shamimu Nyaki.
 
Serikali  kupitia Mpango wa  wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yasiyopewa
kipaumbele leo   imetangaza tarehe 19 hadi 23 mwezi huu kuwa itaanza zoezi la kugawa dawa kwa makundi yanayopaswa kupata dawa za magojwa hayo. 
 
 Tamko  hilo  limetolewa na Katibu mkuu wa Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wazee,na Watoto  Bw. Donald  Mmbando alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Magonjwa  ambayo hayapewi kipaumbele  ni Usubi,Vikope (Trakoma), Matende,Mabusha,Ngiri maji, na Minyoo ya tumbo  hivyo dawa hizo zitasaidia kupunguza tatizo.
 
Ameongeza kuwa zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, shule za msingi na sekondari,sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali na Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi  kupata huduma hiyo ambayo haina malipo yoyote.
 
Katibu Mkuu huyo  amesema kuwa wahusika wakuu katika kupatiwa dawa hizo ni Watu wote kuanzia miaka mitano na kuendelea,isipokuwa watoto chini ya miaka mitano,wajawazito, mama    anaenyonyesha mtoto chini ya siku saba na Wagonjwa Mahututi.
 
“Tunataka kulinda afya zao na Uhai wao hivyo tunaomba wafuate maelekezo vizuri”.Alisema Bw Mmbando.
 
Aidha zoezi hilo litatekelezwa  katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma,Mtwara, Lindi na Pwani kwa ajili ya kujikinga  na kutibu magonjwa hayo na Mikoa mingine iliyobaki itafanya zoezi hilo  katika  ngazi ya
jamii na shuleni mwishoni mwa mwezi Januari kuendelea hadi Februari
2016.
 
Naye Mratibu wa Mpango  huo Dkt Edward kirumbi ameeleza kuwa takwimu zainaonyesha kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele hapa nchini ni kubwa ambapo ugonjwa wa Usubi umeenea zaidi katika mikoa sita ikiongozwa na Dodoma, Ugonjwa wa Minyoo ya tumbo wagonjwa million 13, kichocho ,Matende na Mabusha tathmini za awali zinaonyesha
mikoa 18  imeathirika kwa kuwa na wagonjwa million 12.
 
 Vile vile Dkt Kirumbi ameeleza kuwa Magonjwa haya yamekuwa na athari kubwa hasa kwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa hivyo wananchi wanapaswa kupata dawa hizo ambazo zitakuwa zinatelewa kwa mwaka mara moja  ili kukinga upungufu wa Damu, kuuwa vimeleavya ugonjwa huo, kupungua kwa magonjwa ya ngozi, na kuongeza virutubisho bora mwilini.
 
Hata hivyo jamii inapaswa kupewa elimu zaidi kuhusu Magonjwa haya kwa vile bado haijaelewa athari za magonjwa haya kwa  kiasi kikubwa hasa kwa maeneo ya vijijini ambayo ndio waathirika wakubwa.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yatangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yatangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
http://1.bp.blogspot.com/-mtQ7q6c0QQQ/VnQBFTtUm3I/AAAAAAADcmU/pKePyVuD6Vo/s640/6.JPG
http://1.bp.blogspot.com/-mtQ7q6c0QQQ/VnQBFTtUm3I/AAAAAAADcmU/pKePyVuD6Vo/s72-c/6.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/wizara-ya-afya-maendeleo-ya-jamii.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/wizara-ya-afya-maendeleo-ya-jamii.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago