Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw. Juma-Alfani Mpango.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe.  Juma- Alfani  Mpango  ambaye alikwenda...

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe.  Juma- Alfani  Mpango  ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  nchini, Mhe. Juma-Alfani Mpango ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Mhe. Juma - Alfani Mpango   ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
---
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw. Juma-Alfani Mpango.
 
Akizungumza na balozi Mpango leo (Jumatano, Desemba 2, 2015), ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alimshukuru balozi huyo kwa pongezi zake na kumuomba aendelee kuwa balozi mzuri wa kuitangaza Tanzania hata baada ya kurejea nyumbani.
Pia alitumia fursa hiyo kuwaombea heri wananchi wa DRC pamoja na Rais Joseph Kabila katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika nchini humo mwakani.
 
Kwa upande wake, Balozi Mpango ambaye alisema amekaa hapa nchini kwa miaka 12, alimweleza Waziri Mkuu kwamba amejifunza mengi sana kutoka kwa viongozi wa Tanzania kubwa vikiwa ni uchapakazi na unyenyekevu. “Nimeona utawala wa Rais Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete na sasa Dkt. John Pombe Magufuli. Ninavutiwa na hatua mnazochukua hivi sasa katika kupambana na rushwa na ufisadi,” alisema.
 
“Mambo niliyojifunza tangu nimekaa hapa ni uchapakazi na unyenyekevu. Unaona kabisa kwamba mtu anaamini kuwa madaraka siyo kitu cha kujivunia kwa mtumishi wa umma. Anachotakiwa kuwa nacho ni utayari wa kuwatumikia wananchi,” alisema kwa Kiswahili sanifu.
 
Balozi Mpango aliomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe kwani DRC imekuwa ikinufaika na matumizi ya bandari ya Dar es Salaam katika kusafirishia bidhaa zake kwenda nchi za nje.
 
“Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu sana kwetu. Mwaka 2004 tulisafirisha tani za mizigo 200,000, mwaka 2014 ziliongezeka na kufikia tani milioni 1.3; na mwakani tunataraji zitaongezeka na kufikia tani milioni tatu,” alisema.
 
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, DESEMBA 2, 2015.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw. Juma-Alfani Mpango.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw. Juma-Alfani Mpango.
http://3.bp.blogspot.com/-wERdTHcFYRo/Vl7rcJXNLNI/AAAAAAADbsg/zrbpE8UPsR0/s640/IMGS3649.JPG
http://3.bp.blogspot.com/-wERdTHcFYRo/Vl7rcJXNLNI/AAAAAAADbsg/zrbpE8UPsR0/s72-c/IMGS3649.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-amekutana.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-amekutana.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago