Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA USAFI SOKO KUU LA KARIAKOO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.  Kulia...

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la  Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea eneo la shimoni kwenye soko kuu la Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.  kushoto  kwake ni  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki na Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.
 Baadhi ya washiriki wa zoezi la usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam wakipiga picha kwa kutumia simu wakati Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa alipozunguza nao baada ya kufanya usafi  sokoni hapo  Desemba 9, 2015
Gari alilopanda Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa likitoka kwenye eneo la soko kuu la Kariakoo alikokwenda kushiriki katika kufanya usafi Desemba 9, 2015. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
---
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zoezi la usafi lililofanyika leo nchini kote lisiishie hapo bali liwe endelevu ili Tanzania iwe na taswira nzuri kwa wageni wanaoingia nchini.

Ametoa wito huo leo kwenye soko la Kariakoo wakati akishiriki zoezi la kufanya usafiikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru yasiwepo na badala yake watu wote washiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi wa soko la Kariakoo wafike ofisini kwake Jumatatu ijayo (Desemba 14, 2015) saa 4 asubuhi ili wamueleze wana mikakati gani ya kuboresha utoaji huduma kwenye soko hilo.

“Natambua kuwa siyo sahihi kupanga chini biashara tulizonazo. Nataka hawa viongozi waje wanieleze wana mpango gani endelevu wa kuboresha soko hili,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.

Waziri Mkuu ambaye alienda kufanya usafi kwenye soko hilo,  alilazimika kuzungumza na mamia ya wananchi waliofika kushiriki zoezi hilo. Pia alikagua maeneo mbalimbali ya soko hilo hadi shimoni na kusema aneridhika na usafi uliofanyika bali amesisitiza usafi huo uendelezwe.

“Kaulimbiu ya Mheshimiwa Rais Magufuli ya HAPA KAZI TU inatupa ari ya kufanya kazi. Fanyeni kazi. Watanzania mko huru kufanya kazi yoyote lakini cha msingi fuateni taratibu na kanuni. Serikali hii tumamua kuwajali watu wa chini. Tutahakikisha wajasiriamali wadogo, akinamama lishe na wamachinga mnafanya kazi kwa amani na utulivu, ” alisema.

Rais Magufuli aliamua kuitangaza siku ya leo (Desemba 9, 2015) ambayo ni maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru iwe ni siku ya kufanya usafi nchi nzima ili kuepukana na magonjwa mbalimbali na hasa kipindupindu..

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA USAFI SOKO KUU LA KARIAKOO
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA USAFI SOKO KUU LA KARIAKOO
http://2.bp.blogspot.com/-WAzsJASyb5g/VmhtVZMKZbI/AAAAAAADcKY/OyAlAnRIL1c/s1600/mal2.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-WAzsJASyb5g/VmhtVZMKZbI/AAAAAAADcKY/OyAlAnRIL1c/s72-c/mal2.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-afanya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-afanya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago