Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WAVUVI UKANDA WA PWANI YA BAHARI YA HINDI KUNUFAIKA NA UVUVI WENYE TIJA.

Jovina Bujulu- MAELEZO. 4/12/2015.Dar es Salaam. Wavuvi waishio ukanda wa maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi upande wa Tanzania ...

Jovina Bujulu- MAELEZO.
4/12/2015.Dar es Salaam.

Wavuvi waishio ukanda wa maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi upande wa Tanzania Bara na  Zanzibar  wanatarajia kunufaika na elimu ya ukuzaji viumbe kwenye maji  na teknolojia sahihi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi  kupitia mradi wa Udhibiti wa Uvuvi na Maendeleo Shirikishi  Kusini Magharibi  mwa Bahari  ya Hindi  (SWIOFISH).

Hayo yamesemwa  jijini Dar es salaam  na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bi. Fatma Sobo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa  Udhibiti Uvuvi na Maendeleo Shirikishi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi, ulioanza kutekelezwa  mwezi Juni mwaka huu.

Amesema lengo la mradi huo ni kuwasaidia wavuvi wadogo wa ukanda huo ili waweze kunufaika na shughuli hiyo na kuwa na uvuvi  endelevu wenye kuongeza faida kiuchumi, kijamii na kimazingira.

‘Lengo la mradi huu ni kuhakikisha kuwa wavuvi wa ukanda wa Pwani wanakuwa na uvuvi endelevu na wananufaika na rasilimali za bahari kwa kuimarisha uwezo wa Taasisi za Kikanda na Serikali” Amesema.
Ameeleza kuwa katika kufuatilia utekelezaji wa mradi huo , Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,imeanzisha mpango  wa uongozi na usimamizi wa uvuvi ambapo wavuvi wanapatiwa elimu kuhusu aina za samaki, aina ya nyavu za kuvulia, muda wa kuvua, mauzo na uhifadhi wa samaki. 

Ameongeza kuwa mradi huo utaimarisha mfumo wa taarifa za uvuvi  kama vile mavuno, nguvu ya uvuvi inayotumika , mauzo ya ndani na  nje nchi yatokanayo na shughuli hizo.

Bi. Fatma aliongeza kuwa kipaumbele cha mradi huo kimewekwa katika uvuvi wa samaki aina ya pelagiska, Jodari, Kamba miti, samaki mwamba, pweza na ukuzaji  viumbe kwenye maji bahari ambapo eneo la majaribio litakuwa katika wilaya za Mkinga, Pangani, Tanga, Bagamoyo mjini na Lindi Vijijini.

Aidha, amesema mradi huu utatekelezwa kwa miaka 6, kuanzia 2015 hadi 2021 na umefadhiliwa na Mfuko wa Mazingira Duniani na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo kwa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 36,000 ambapo utazihusisha wilaya 16 kutoka ukanda wa bahari ya Hindi, mkoa wa Tanga  hadi Mtwara.
Ameongeza kuwa mradi huo ukizishirikisha Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi (Tanzania Bara), Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Zanzibar) na Mamlaka ya Kusimamia Bahari Kuu utakomesha uvuvi haramu wa kutumia Mabomu. 

Taasisi zitakazotelekeza mradi huo ni Wakala wa Mafunzo ya Elimu ya Uvuvi, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Vikundi vya Ujasiriamali na Jamii za watu wa Pwani.

MWISHO

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WAVUVI UKANDA WA PWANI YA BAHARI YA HINDI KUNUFAIKA NA UVUVI WENYE TIJA.
WAVUVI UKANDA WA PWANI YA BAHARI YA HINDI KUNUFAIKA NA UVUVI WENYE TIJA.
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/wavuvi-ukanda-wa-pwani-ya-bahari-ya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/wavuvi-ukanda-wa-pwani-ya-bahari-ya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago