Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

URUWA Yaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano

 Mwenyekiti wa Umoja wa Rufaa ya Wananchi (URUWA) John Shibuda(katikati) akisistiza jambo kwa waandishi wa Habari wakati umoja huo wal...

 Mwenyekiti wa Umoja wa Rufaa ya Wananchi (URUWA) John Shibuda(katikati) akisistiza jambo kwa waandishi wa Habari wakati umoja huo walipokuwa wakitoa pongezi kwa Rais wa Awamu ya Tano.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Rufaa ya Wananchi (URUWA) John Shibuda akitoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Rufaa ya Wananchi (URUWA) John Shibuda(katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakimpongeza Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli kwa uongozi uliotukuka (Kulia) ni mjumbe wa umoja huo Kaimu Katibu Mkuu – UDP Isaac Cheyo, wa pili kushoto Katibu Mkuu wake  Mwenyekiti Taifa – UPDP Fahami Nassoro Dovutwa na kushoto ni mjumbe wa umoja huo Makamu Mwenyekiti- SAU Yusuf Salum Manyanga.Picha Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
----
Na Lilian Lundo MAELEZO
Uongozi unaounda mashirikiano ya umoja wa vyama visivyo na Ruzuku ya Serikali ambavyo ni  ADA-TADEA, UDP, UPDP na SAU uitwao URUWA (Umoja wa Rufaa ya Wananchi) umeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uongozi uliojaa utukufu wa uzalendo.
 
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa URUWA John Shibuda leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongeo na waandishi wa habari.
“Tunamuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za utumishi aminifu na tiifu kwa ustawi na maendeleo ya Jamii na Taifa, hongera sana kwa uongozi wako uliojaa utukufu wa uzalendo na Neema ya kauli aminifu ya HAPA KAZI TU ambayo ipo kwa maslahi ya Tanzania,” alisema Shibuda.
 
Umoja huo pia umepongeza mshikamano wa uzalendo na uwajibikaji makini unaotekelezwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu  Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
 
Shibuda aliongeza kwa kusema kuwa wananchi wa makundi yote yasiyotarajia kuingia katika kundi la uchumi wa kati sasa wanamatumaini ya kufikia uchumi wa kati kutokana na kupata utumishi sikivu kwa vilio vyao vya muda mrefu vya kupata maisha bora.
 
Aidha, uongozi wa umoja huo umesema kwamba unaunga mkono juhudi zote zinazotekeleza Serikali ya Awamu ya Tano katika kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jamii na Taifa. Pia wameitaka Serikali ya Awamu ya Tano kuendelea kutakatisha na kung’arisha usafi wa mazingira ya uwajibikaji wa safari ya ukombozi ya ASP na TANU.
 
Umoja wa vyama visivyo na Ruzuku ya Serikali URUWA umeundwa tarehe 18/12/2015  huku Mwenyekiti wa Umoja huo akiwa ni John Shibuda  ambaye ni Katibu Mkuu- ADA-TADEA, Katibu Mkuu akiwa ni Fahami Nassoro Dovutwa ambaye ni Mwenyekiti Taifa – UPDP.
 
Wajumbe wa umoja huo ni Isaac Cheyo ambaye  Katibu Mkuu – UDP, Paul Kyara   Mwenyekiti SAU na Yusufu Manyanga  ni Makamu Mwenyekiti – SAU.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: URUWA Yaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano
URUWA Yaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano
http://4.bp.blogspot.com/-zEcMnerazYU/VnlNki4zIII/AAAAAAADcwg/zRjrF9LSo5o/s640/ur3.jpg
http://4.bp.blogspot.com/-zEcMnerazYU/VnlNki4zIII/AAAAAAADcwg/zRjrF9LSo5o/s72-c/ur3.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/uruwa-yaipongeza-serikali-ya-awamu-ya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/uruwa-yaipongeza-serikali-ya-awamu-ya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago