Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

UNODC YAKABIDHI VIFAA VYA MAABARA JESHI LA MAGEREZA

Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Immaculata Nyoni akizungumza jam...


Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Immaculata Nyoni akizungumza jambo kabla ya kukabidhi vifaa vya maabara kwa Jeshi la Magereza nchini.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya maabara kwa Magereza Tanzania.
DSC_0126
Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Immaculata Nyoni pamoja na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa vifaa vya maabara vilivyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC).
Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Immaculata Nyoni akitolea ufafanuzi vifaa vya maabara alivyokabodhi kwa Jeshi la Magereza ili kusaidia kuwapima wafungwa walioko magerezani.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa shukrani baada ya kupokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) lililowakilishwa na Immaculata Nyoni.
Hivi ndivyo vifaa vya maabara vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza.
Picha ya pamoja. Na Mwandishi wetu Jeshi la Magereza Ukonga limepokea vifaa vya maabala kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) ambavyo vitasaidia kutoa vipimo kwa wafungwa waliofungwa magerezani hii ikiwa ni jitihada za kupunguza matumizi ya dawa za kulevya katika magereza hapa nchini. Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Bi. Immaculata Nyoni ambaye ni Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) alisema wametoa msaada huo baada ya kufanyika kwa tafiti hasa kwenye magereza hapa nchini na utafiti huo Magereza ilishirikiana na UNODC na kubaini changamoto wanazozipata wafungwa wakati wa kupimwa afya zao. 

Hivyo kama shirika limeamua kutoa msaada wa vifaa vya maabala ambavyo ni Hematology mbili(2), Urine Analyzer tatu (3) pamoja na Hemoglobin Mashine mbili(2) na vifaa hivi vimegharimu takribani shilingi milioni 10 za kitanzania. Akitoa shukrani Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa kwa niaba ya Mkuu wa Magereza hapa nchini amesema anawashukuru UNODC kwa kuona matatizo yanayowakabili hasa kwenye hospitali za Magereza zinazohudumia wafungwa na kuamua kutoa msaada huo kwa jeshi hilo.

  Pia alisisitizaushirikiano kati ya Jeshi la Magereza pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) kuimarishwa ili kuweka ukaribu kwa kila jambo linalohusu afya ya wafungwa hasa kwa wale waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya na wenye virusi vya UKIMWI. Baada ya wauguzi kupokea msaada huo walisema sasa ni muda wa kazi tu kwani wamepata vifaa ambavyo vitaweza kuwahudumia wagonjwa kwa wakati kwani hapo mwanzo kulikuwa na uhaba wa vifaa vya maabara na kupelekea matibabu kutokuwa ya uhakika katika hospitali za Magereza zinazohudumia wafungwa.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: UNODC YAKABIDHI VIFAA VYA MAABARA JESHI LA MAGEREZA
UNODC YAKABIDHI VIFAA VYA MAABARA JESHI LA MAGEREZA
http://2.bp.blogspot.com/-E9WGUtcAY3k/VmvwR_gM-rI/AAAAAAABaE8/RAh5lWSl0-E/s640/DSC_0103.JPG
http://2.bp.blogspot.com/-E9WGUtcAY3k/VmvwR_gM-rI/AAAAAAABaE8/RAh5lWSl0-E/s72-c/DSC_0103.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/unodc-yakabidhi-vifaa-vya-maabara-jeshi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/unodc-yakabidhi-vifaa-vya-maabara-jeshi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago