Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Taarifa Kwa Umma Kutoka IKULU:Rais Dr John Magufuli atuma salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Askofu Nkalanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu Mstaafu Plasdus Gervas Nkalanga (OSB) kilichotokea Ijumaa tarehe 18 Desemba, 2015 katika hospitali ya Mtakatifu Joseph Peramiho, Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.Mhashamu Askofu Nkalanga aliyekua Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba alistaafu uaskofu mwaka 1974 na kujiunga na watawa wabenediktini wamonaki ambapo aliamua kwenda kuishi katika Abasia ya Hanga iliyopo katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.  Katika salamu zake Rais Magufuli amesema  Askofu Nkalanga aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96 atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kuhimiza imani na uchapakazi kazi katika kipindi chote cha miaka 54 ya uaskofu wake na utawa wake akiwa katika Abasia ya Hanga.Amesema Marehemu Askofu Nkalanga ambaye baada ya kustaafu aliamua kuingia katika utawa akianzia katika ngazi ya chini kabisa ya Unovisi hadi alipofunga nadhili za milele za utawa mwaka 2009, ameacha mfano mzuri unaohimiza jamii kuishi kwa upendo, unyenyekevu na kutokata tamaa. "Kupitia kwako Baba Askofu Ngalalekumtwa napenda kuwapa pole nyingi Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Abate wa Abasia ya Hanga, watawa na waumini wote wa kanisa Katoliki kwa kupoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kanisa na jamii kwa ujumla" amesema Rais Magufuli.Rais John Pombe Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu Mhashamu Askofu Mstaafu Plasdus Gervas Nkalanga mahali pema peponi, Amina.
Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

20 Desemba, 2015

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Taarifa Kwa Umma Kutoka IKULU:Rais Dr John Magufuli atuma salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Askofu Nkalanga
Taarifa Kwa Umma Kutoka IKULU:Rais Dr John Magufuli atuma salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Askofu Nkalanga
http://2.bp.blogspot.com/-hyCOwPeO62I/VnfprT_uMSI/AAAAAAADcsA/L8ntbizWtbo/s640/20151126022044.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-hyCOwPeO62I/VnfprT_uMSI/AAAAAAADcsA/L8ntbizWtbo/s72-c/20151126022044.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/taarifa-kwa-umma-kutoka-ikulurais-dr_21.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/taarifa-kwa-umma-kutoka-ikulurais-dr_21.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago