Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

PICHA NA TAARIFA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KWA WATANZANIA ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO OFISINI KWAKE KUHUSU RAIS DR JOHN MAGUFULI KUMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA BANDARI AWADHI MASSAWE NA KUTENGUA UTEUZI WA KATIBU MKUU UCHUKUZI,NA KUVUNJA BODI YA MAMLAKA YA BANDARI-TPA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kwa waandishi wa habari, ripoti Bandari ya Dar es salaam iliyobaini mianya ya ukwepaji kodi iki...

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kwa waandishi wa habari, ripoti Bandari ya Dar es salaam iliyobaini mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
1 
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa  akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo wakati alipotoa taarifa ya serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi wa TPA, TRA, Wizara ya Uchukuzi na TRL. kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni Sefue. 
---
Mnamo tarehe 27 Novemba, 2015 nilifanya ziara ya kushitukiza Bandari ya Dar es Salaam ambapo nilifichua mwanya wa ukwepaji kodi kwa makontena 329 yaliyopitishwa bandarini kinyume cha utaratibu.

Mtakumbuka pia tarehe 4 Desemba, 2015 nilirudi tena kufanya ufuatiliaji wa hatua ya udhibiti wa upitishaji wa bidhaa mbalimbali kinyume cha utaratibu.

Ziara yangu ilinipitisha hatua zote za upitishaji mizigo ambazo pia kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi wa Ndani wa tarehe 30 Julai 2015 Mamlaka ya Bandari uligundua kuwepo kwa mianya mingi ya ukwepaji kodi ikiwemo na makotena 2387 yaliyopitiahwa kati ya Machi – Septemba 2014 kinyume cha utaratibu, vitendo hivi vinaonyesha kuwa bandari yetu hupitisha makontena mengi bila ya kulipiwa kodi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.

Upotevu huo unaenda sambamba na mfumo usiokidhi wa kupokelea malipo (BILLING SYSTEM) ambao unatoa mwanya mkubwa wa kupoteza mapato ya Serikali. Bandari ni eneo muhimu ambako kama panasimamiwa vizuri panaweza kukusanya fedha nyingi na kuchangia Pato la Taifa.
Serikali haitavumilia kuona watu wachache au kikundi chochote kilichojipanga kuhujumu mifumo au kuiibia Serikali kwa namna yoyote ile kwa manufaa ya wachache.

Matokeo ya ziara hizo ni haya yafuatavyo:- 1. Nimeagiza mfumo wa kupokelea malipo ubadilishwe kutoka Billing System na uwekwe mfumo wa e-payment ambao tayari ulianza kuwekwa na uwe umekamilika kufikia tarehe 11 Disemba 2015. 2. Kwa kuwa ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji makontena hayo na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, kuanzia muda huu nawasimamisha kazi wale wote waliohusika kupitisha makontena kinyume na utaratibu.
1. Wasimamizi wa Bandari Kavu (ICD) (i) Happygod Naftari (ii) Juma Zaar (iii) Steven Naftari Mtui (iv) Titi Ligalwike (v) Lydia Prosper Kimaro (vi) Mkango Alli (vii) John Elisante
 
(viii) James Kimwomwa – ambaye amehamishiwa Mwanza.
2. Wafuatao ni Viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya Bandari ambao hawamo kwenye ripoti ila ni wahusika wakuu.

1. Shaban Mngazija – Aliyekuwa Meneja Mapato ambaye kwa sassa amehamishiwa Makao Makuu kitengo cha Fedha.
  2. Rajab Mdoe – Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu (ICD) – ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi Co-operate Services. 3. Ibin Masoud – Kaimu Mkurugenzi wa Fedha. 4. Apolonia Mosha – Meneja Bandari Msaidizi – Fedha. 5. James Kimwomwa.

Kutokana na utendaji mbovu wa Mamlaka ya Bandari kwa muda mrefu na kwa kitendo cha kutochukua hatua kwenye vyanzo.

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amevunja Bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa wafuatao:-
1. Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari – Prof. Joseph Msambichaka. 2. Mkurugenzi Mkuu wa Bandari – Bw. Awadhi Massawe.
Ndugu Waandishi wa Habari mtakumbuka pia nilifanya ziara pia TRL ambako kwa awali nimegundua matumizi mabaya ya fedha Shilingi Bilioni 13 nje ya utaratibu ambako uchunguzi unakamilishwa.

Mheshimiwa Rais, pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia tarehe ya leo na atapangiwa kazi nyingine.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: PICHA NA TAARIFA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KWA WATANZANIA ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO OFISINI KWAKE KUHUSU RAIS DR JOHN MAGUFULI KUMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA BANDARI AWADHI MASSAWE NA KUTENGUA UTEUZI WA KATIBU MKUU UCHUKUZI,NA KUVUNJA BODI YA MAMLAKA YA BANDARI-TPA
PICHA NA TAARIFA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KWA WATANZANIA ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO OFISINI KWAKE KUHUSU RAIS DR JOHN MAGUFULI KUMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA BANDARI AWADHI MASSAWE NA KUTENGUA UTEUZI WA KATIBU MKUU UCHUKUZI,NA KUVUNJA BODI YA MAMLAKA YA BANDARI-TPA
http://2.bp.blogspot.com/-7dZ8cdzOfoI/VmWA4oiSRzI/AAAAAAADb98/11gRYcniznc/s640/IMG_6972.JPG
http://2.bp.blogspot.com/-7dZ8cdzOfoI/VmWA4oiSRzI/AAAAAAADb98/11gRYcniznc/s72-c/IMG_6972.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/picha-na-taarifa-taarifa-ya-waziri-mkuu.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/picha-na-taarifa-taarifa-ya-waziri-mkuu.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago