Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango atembelea TRA

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji Naibu Waziri wa Fedha akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na menejiment...

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji
Naibu Waziri wa Fedha akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na menejimenti ya TRA. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bw. Benard Mchomvu na Kushoto kwake ni Naibu Kamishna Mkuu Bw. Lusekelo Mwaseba.
---
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji ametembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufahamiana na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Uongozi wa TRA na kusisitiza msimamo wa serikali ya awamu ya tano katika suala zima la ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya TRA, Dr. Kijaji pamoja na kutoa pongezi kwa TRA kwa jukumu kubwa la kukusanya mapato, ameomba ushirikiano kutoka kwa Bodi na Uongozi wa TRA ili kuweza kuivusha Tanzania salama. Ameongeza kuwa kuwepo ushirikiano kutasaidia TRA kuweza kufikia malengo ya serikali ya kukusanya kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

“Bila mapato hakuna taifa linalosonga mbele”, alisema Naibu Waziri ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Servacius Likwelile. Amesema nchi inategemea mapato kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi na hivyo kuwaongezea wananchi matumaini kwa kuwafikishia huduma muhimu.

Ameutaka uongozi wa TRA kushikamana na kuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya “Hapa Kazi Tu” kwa kusimama imara na kuwabaini wale wanaoichafua TRA na kuwachukulia hatua za kisheria. “Tusikubali wachache wanaotuchafua waendelee kutuchafua”, amesisitiza Naibu Waziri.

Dr. Kijaji amesema kwamba ili wafanyabaishara waifurahie TRA ni lazima kuimarisha ushirikiano kati yake na wafanyabiashara.

Ili kuzidi kuongeza makusanyo, Naibu Waziri ameshauri kuwa misamaha itolewe kwa vigezo, kuimarisha makusanyo yatokanayo na madini. “Tukusanye kodi maeneo yote yanayostahili ili kupunguza utegemezi. Hakuna haja ya kupiga magoti kwa wahisani”, alisema Naibu Waziri na kuongeza kuwa serikali itaendelea kusimamia mazingira ya uchumi na kuhakikisha hakuna kodi ambazo zinakatisha tamaa wawekezaji.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA Bw. Benard Mchomvu amempongeza Naibu Waziri kwa niaba ya wafanyakazi wa TRA kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge na hatimaye kuteuliwa na Rais kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.

Naye Kaimu Kamishna Mkuu Dr. Philip Mpango amemweleza Naibu Waziri kwamba TRA ina wataalamu wazuri wa kodi na inakitumia vizuri Chuo cha Kodi kufundisha wafanyakazi ambao wengi wanakuwa wataalamu wa kodi. Amesema wafanyakazi wanaogundulika kukiuka taratibu za kazi wanachukuliwa hatua lakini wengine wanachapa kazi kwa kufanya jitihada za kukusanya mapato yanayoendana na uchumi wa nchi yetu. “Wafanyakazi wa TRA wanaipenda nchi yao”, amesema Kaimu Kamishna Mkuu.

Kuhusu kufikia lengo la makusanyo hadi Desemba mwaka huu, Dr. Mpango amesema anaimani idara zote za TRA zitafikia malengo. “Matarajio ni kujitahidi kukusanya na kufikia trilioni 1. 3 mwishoni mwa mwezi Desemba” alisema Naibu Kamishna Mkuu.
  Ziara ya Naibu Waziri Dr. Kijaji ni ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika wadhifa huo.
 
Richard Kayombo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Simu: +25522-2119343 Barua pepe: huduma@tra.go.tz

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Naibu Waziri wa Fedha na Mipango atembelea TRA
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango atembelea TRA
http://4.bp.blogspot.com/-QhGXNrqWiBA/VnP_nxRthXI/AAAAAAADclE/VI-WBsLyEec/s640/721.jpg
http://4.bp.blogspot.com/-QhGXNrqWiBA/VnP_nxRthXI/AAAAAAADclE/VI-WBsLyEec/s72-c/721.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/naibu-waziri-wa-fedha-na-mipango.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/naibu-waziri-wa-fedha-na-mipango.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago