Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MKOA WA MBEYA WATEKELEZA AGIZO LA RAIS KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA TIBA KWA FEDHA ZA MAADHIMISHO YA UKIMWI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Dkt Magufuli kuhu...


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Dkt Magufuli kuhusu   Ununuzi wa Vifaa tiba pamoja na Dawa za ARV kutoka katika fedha zilizochangishwa na wadau kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya Ndugu Stella Kategile akitoa taarifa ya UKIMWI kwa mkoa wa Mbeya kwa ujumla wake.
Dawa pamoja na vifaa tiba vilivyo nunuliwa kutoka katika fedha zilizo changishwa na wadau kwa ajili ya Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kushoto akimkabidhi Mganga Mkuu mkoa wa Mbeya Dkt Sefu Mhina  moja ya  vifaa tiba vilivyonunuliwa na  kutoka katika fedha zilizo changishwa  na wadau kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani.Picha Keneth Ngelesi.
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Siku chache mara baada ya Serikali kutangaza kuahirisha shughuli za maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo yalipangwa kufanyika Kitaifa mkoani Singida mwaka huu na badala yake pesa hizo zikatumike kununua Vifaa tiba pamoja na Dawa za ARV hatimaye agizo hilo limetekelezwa na uongozi wa Mkoa wa Mbeya . 

Akizungumza na waandishi wa habari  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbasi kandoro, amesema pesa zilizokusanywa na kamati ya inayoratibu maadhimisho hayo kwa mkoa wa mbeya  ni  kiasi cha shilingi milioni 3.5 ambazo zimetumika kwa ajili ya kutekeleza agizo hilo la rais Magufuli kwa ununuzi wa ununuzi wa vifaa tiba pamoja na dawa hizo za ARV.

Amesema, kiasi hicho cha fedha kilipatikana baada ya wahisani mbalimbali kuchangia na kwamba kiongozi huyo amewataka wadau ambao hawakupata fursa ya kuchangia waendelee kwani mahitaji bado ni makubwa hususani katika suala nzima la chakula.

Aidha, Mkuu huyo alitoa shukrani za pekee kwa kanisa la Anglikan mkoa wa Mbeya kwa kuchangia boksi saba za kondomu na kuwataka wananchi kuendelea kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa wa ukimwi kwani hali ya takwimu bado si nzuri kwa Mkoa wa Mbeya.

Akizungumzia hali ya ugonjwa wa ukimwi kimkoa, Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa, Stella Kategile, alisema kuwa  kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa kitaifa hali ya maambuki kwa VVU na UKIMWI uliofanyika mwaka 2011/2012 unaonyesha Mkoa wa Mbeya unamaambukizi asilimia 9.0 ambayo ni juu ya wastani wa kitaifa wa asilimia 5.1.

Hata hivyo, Kategille alitoa wito kwa wananchi  kushirikiana kwa hali na mali katika kutokomeza ugonjwa huo wa UKIMWI kwenye jamii na hatimaye kutimiza kauli mbiu ya “Tanzania bila ya Maambukizi mapya ya VVU, vifo vitokanavyo na ukimwi pamoja na unyanyapaa dhidi ya wagonjwa inawezekana.
Mwisho.

 (JAMIIMOJABLOG-MBEYA) 

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MKOA WA MBEYA WATEKELEZA AGIZO LA RAIS KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA TIBA KWA FEDHA ZA MAADHIMISHO YA UKIMWI
MKOA WA MBEYA WATEKELEZA AGIZO LA RAIS KUHUSU UNUNUZI WA VIFAA TIBA KWA FEDHA ZA MAADHIMISHO YA UKIMWI
http://4.bp.blogspot.com/-B-vC43EY_ig/Vl8BZEpySaI/AAAAAAAAU1c/qyvilq8f7QU/s640/IMG_4772.JPG
http://4.bp.blogspot.com/-B-vC43EY_ig/Vl8BZEpySaI/AAAAAAAAU1c/qyvilq8f7QU/s72-c/IMG_4772.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/mkoa-wa-mbeya-watekeleza-agizo-la-rais.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/mkoa-wa-mbeya-watekeleza-agizo-la-rais.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago