Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

KONGAMANO LA MSAFARA LILILOFANYIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM LAWAJENGA VIJANA WENGI

  Msanii wa sanaa za Maonesho Vanensia Shule, ambaye pia ni Mkufunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam upande wa sanaa na Filamu akielez...


 Msanii wa sanaa za Maonesho Vanensia Shule, ambaye pia ni Mkufunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam upande wa sanaa na Filamu akielezea jinsi Sanaa inavyoweza kumkomboa kijana,na kutoa mifano ya baadhi ya wasanii walioanzia chini na sasa wanamafanikio makubwa.
Baadhi ya vijana wakionesha ishara ya ushindi
Alphonse Matata ambaye anajihusisha na kilimo pia Mjasiliamali kupitia ufugaji wa nyuki akielezea safari yake ya mafanikio ,na kuwashauri vijana wasingoje kuajiliwa bali wawe wabunifu na kujiunga katika ujasiliamali, jana tarehe 4.12.2015
 MC Suhaila Thawer akiendelea kutoa utaratibu wa wazungumzaji 
Mjasiliamali Maarufu na Mtoa ushauri wa biashara na mambo mbalimbali James Mwang'amba, alitoa Historia ya Maisha yake na kutoa siri tatu za mafanikio ambazo ni kuwa na maono ya maisha bora ya baadae, kujifunza kwa kupitia njia mpya ya Teknolojia mfano youtube na kuwa na mtu ambaye unahisi unaweza ukajifunza kwake.
 Baadhi ya vijana wakifuatilia Kongamano hilo
 Aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wanawake 2002-2003 na kuchezea mpira timu hiyo kwa Miaka 15 mpaka anastaafu mwaka huu Esther Chabruma akielezea namna mchezo wa Mpira wa Miguu ilivyoweza msaidia mpaka hapa alipofikia na kuwasihi vijana wasikate tamaa maana kila jambo lina wakati wake
 Baadhi ya vijana wakiwa wanasikiliza kwa makini vijana wenzao wakielezea safari zao za mafanikio
 Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam Kitaponda Ahadi, akielezea kuhusu elimu na changamoto alizo zipata wakati wa akiwa Shule mpaka ndoto yake ilivyotimia ya kuja kusoma chuo kikuu na kuwa kiongozi, amewasihi vijana wenzake wasikate tamaa wafanye bidii katika masomo watafikia malengo.
  Major Mbuya mtaalam wa kuendesha Baiskeri na mwanzilishi wa waendesha Baiskeri Tanzania, akielezea jinsi ubunifu ulivyo msaidia mpaka sasa amefanikiwa
 Hassan ally kijana mjasiliamali akieleza namna alivyoweza kubadilisha taka na kuwa Bidhaa ambayo inaweza kutumika tena kwa matumizi mengine pia, ameelezea mpango wake wa kuanza kujenga nyumba kwa kutumia bei nafuu.

Vijana mbalimbali wamejitokeza katika kongamano la msafara kusikiliza baadhi ya vijana wenzao ambao wametoa historia zao kuhusu walipotokea mpaka wamefanikiwa kufika hapo walipofikia na kuwatia moyo vijana wengine wasikate tamaa kwa sababu mafanikio yapo.

Msafara ambao unalenga kuibua na kurudisha ndoto za vijana katika sekta zote kwa kutambua kuwa kila eneo lina mchango mkubwa katika mafanikio na maendeleo ya vijana. Wazungumzaji tofauti tofauti walijikita katika maeneo makuu yafuatayo Sayansi na Teknolojia,Kilimo, Biashara, Sanaa na usanii, Elimu, Uongozi, Michezo, utunzaji Mazingira, haki sawa za kijinsia pamoja na harakati.

Maeneo hayo yalikuwa ni nguzo kuu ya kufanya vijana kuwa na fursa ya kukabiliana na changamoto za kimaisha katika kufikia mafanikio na malengo yao. Katika safari hii ya Msafara matukio mbalimbali yatafanyika ikiwemo kuwaleta vijana wa rika moja wenye umri wa miaka 15-24 ili kuwaleta kwa pamoja wapate kujifunza kutoka kwa wengine waliofanikiwa, wenye fani mbalimbali/Taaruma zao, hii itawajengea ujasili wengine katika kufikia mafanikio yao.

Progamu hii inaendeshwa na muungano wa Mashirika na Makundi Matano yaliyopo hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na DARUSO, YouthCAN, NGAO YOUTH na Young Feminist Forum na inaratibiwa na Oxfam Tanzania, msafara itakuwa ni moja ya fursa kwa vijana kutangaza na kuonesha ubunifu wao na mafanikio waliyofikia kimaisha ingawa kuna changamoto na vikwazo mbalimbali. Safari ya msafara itaendelea Ifakara mkoani Morogoro tarehe 12.12.2015

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: KONGAMANO LA MSAFARA LILILOFANYIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM LAWAJENGA VIJANA WENGI
KONGAMANO LA MSAFARA LILILOFANYIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM LAWAJENGA VIJANA WENGI
http://4.bp.blogspot.com/-lgjRPdMQZNs/VmG6iMSxs5I/AAAAAAAAeaw/n_9jO7BzPOY/s640/1a.JPG
http://4.bp.blogspot.com/-lgjRPdMQZNs/VmG6iMSxs5I/AAAAAAAAeaw/n_9jO7BzPOY/s72-c/1a.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/kongamano-la-msafara-lililofanyika-chuo.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/kongamano-la-msafara-lililofanyika-chuo.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago