Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Kichupa cha 'Utanipenda' cha Diamond nyuma ya pazia

Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kasimama mbele ya magari aliyoyatumia katika video yake mpya ya Utanipenda. Staa ...

Diamond platinumz (4)
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kasimama mbele ya magari aliyoyatumia katika video yake mpya ya Utanipenda.
Diamond platinumz (10)Staa wa Bongo, Jacqueline Wolper, akiongea jambo na Diamond.
Diamond platinumz (7)Gari ya Wolper katika video hiyo ikimmwagia maji Diamond.
Diamond platinumz (5)
Diamond akiangalia vipande vya video hivyo kabla ya kuendelea kushuti.
Diamond platinumz (8)Diamond akiangalia Magazeti Pendwa baada ya kupata matatizo, nayo hayakuwa nyuma kuandika.
Diamond platinumz (1)Diamond akipiga kinanda huku akimuimbia mpenzi wake Zari.
Diamond platinumz (12)Mama yake Diamond, Sanura Kasim (kushoto) akifukuzwa na mlinzi baada ya kwenda kuomba msaada kwa JK.
Diamond platinumz (11)Diamond akiongea jambo.
Diamond platinumz (2)Diamond akiwa kapozi na mpenzi wake Zari.
Sasa hivi kwenye ulimwengu wa muziki, gumzo ni ngoma aliyoitoa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayokwenda kwa jina la Utanipenda. Ni ngoma kali ambayo itatambulishwa kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar. Mbali na utambulisho wa ngoma hii ambayo itapigwa live kwa kutumia vyombo, nyimbo nyingine ambazo Diamond atazipiga siku hiyo ni pamoja na Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyinginezo zinazobamba huku akiwa na madansa wake kutoka Wasafi Classic Baby (WCB). Itakuwa ni siku ya Krismasi (Ijumaaa ijayo) ambayo msanii huyo ameahidi kufanya mambo makubwa akisindikizwa na mkali wa nyimbo za Singeli, Msaga Sumu pamoja na wacheza dansi hatari Afrika Mashariki, Wakali Dancers na wasanii wengine kibao. 

Burudani yote hiyo ambayo imedhaminiwa na huduma kutoka kampuni ya simu Tanzania, Airtel Money utaipata kwa kiingilio cha shilingi 15,000 tu getini na wale watakaohitaji huduma ya VIP watalipia shilingi 30,000. Katika kuelekea kwenye shoo hiyo, Showbiz ilifanikiwa kunasa baadhi ya picha za nyuma ya pazia ‘behind the scene’ wakati kichupa cha wimbo huo kikiandaliwa. Video hiyo ni mkono wa yuleyule mkali wa vichupa kutoa Sauzi anayekwenda kwa jina la God Father. Hajakosea! Amefanya bonge la kazi na hata mashabiki ni mashahidi kwamba wimbo ni mkali na kideo chenyewe ni ‘kitamu’. Maneno mengi siyo ishu, kwenye hili picha zinaongea zaidi hivyo pitisha macho kwenye baadhi ya picha hizo ili upate uhondo! Kwani kuna mtu kaibiwa? Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Kichupa cha 'Utanipenda' cha Diamond nyuma ya pazia
Kichupa cha 'Utanipenda' cha Diamond nyuma ya pazia
http://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2015/12/Diamond-platinumz-4-1024x683.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/kichupa-cha-utanipenda-cha-diamond.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/kichupa-cha-utanipenda-cha-diamond.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago