Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando afungua rasmi duka la dawa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambalo linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando (wa pili kutoka kushoto) akifungua duka la dawa leo katika Ho...


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando (wa pili kutoka kushoto) akifungua duka la dawa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambalo linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi  wa MNH, Profesa Lawrence Mseru.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando akipewa taarifa ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu kufungua duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua duka la dawa linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).  Duka hilo limefunguliwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). 
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa duka la dawa la MSD.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja leo katika hospitali hiyo baada ya kufunguliwa kwa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) leo jijini Dar es Salaam.
 Mwonekano wa Duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) .Picha zote kwa hisani ya
Msimamizi wa duka hilo, Betia Kaema (kushoto), akitoa maelezo kwa  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (wa pili kulia), akimsikiliza Msimamizi wa Duka hilo, Betia Kaema (hayupo pichani), wakati wa ufunguaji wa duka hilo. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, Profesa Idrisa Mtulia, Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Laurence Mselu na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu.
Mwonekano wa duka hilo kwa nje.
Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD, Salome Malamia (kulia), akizungumza na wateja waliofika kuhudumiwa katika duka hilo.
Maofisa wa MSD wanaotoa huduma katika duka hilo wakiwa kazini.
Dawa zikiwa zimepangwa katika duka hilo.
Wateja wakiwa katika duka hilo.
Msimamizi wa duka hilo, Betia Kaema, akitoa maelezo kwa  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando wakati akikagua duka hilo.
--
Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imesema haiwezi kufunga maduka ya Dawa binafsi yaliyopo nje ya hospitali hapa nchini na badala yake kuimarisha upatikanaji wa huduma za dawa katika duka la bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali hizo.

Hali hiyo imefika kutokana na agizo la rais John Magufuli wakati alipofanaya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam Novemba 9 mwaka huu.

Akizungumza jijini humo wakati wa uzinduzi wa Duka la Bohari ya Dawa (MSD) hospitalini hapo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mbando alisema upatikanaji wa duka hilo hospitalini hapo kutapunguza adha za wagonjwa wanaohitaji dawa.

"Kufunguliwa kwa duka hili kutapunguza wagonjwa walikuwa wakilalamika na kutaabika ambapo kutokana na hali hiyo wakati wa ziara yake rais alitoa agizo la kuwepo kwa duka hili ndani ya hospitali,"alisema.

Alisema wateja wakuu katika duka hilo ni serikali na hospitali za serikali ambapo mgonjwa akitaka dawa huelekezwa na kupewa karatasi maalumu kwa ajili ya manunuzi ya dawa hizo dukani humo.

"Dawa zenye majina mengi zitapatikana hapa. Tutalisimamia na tutafurahi zaidi tukipata mrejesho kutoka kwa wananchi, matarajio yetu ni kupata mahitaji yote ya dawa tofauti tofauti,"alisema Dk.Mmbando.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MSD, Laurrean Bwanakunu alisema kazi kubwa ya bohari hiyo ni kununua, kuuza na kusambaza dawa kwa serikali na kujipanga kutoa huduma hiyo katika hospitali zote za kanda.

Ofisa Udhibiti Ubora (MSD), Betia Kaema alisema hospitali za serikali zinapaswa kupeleka oda za dawa ambazo wanahitaji ili kuepusha usumbufu wa kutopatikana kwa dawa 
katika duka hilo.

"Tunajidhatiti katika kutoa huduma kwa saa 24, Muhimbili watoe mahitaji yao ya dawa mapema ili kusiwe na usumbufu wa upatikanaji wa dawa,"alisema Kaema 

Kaema alifafanue zaidi kuwa dawa zinazopatika katika duka hilo na za bei nafuu ukilinganisha na gharama za duka la dawa binafsi.

"Nitoe mfano mdogo tu jana alikuja mteja hapa aliandikiwa dawa na daktari aje kununua hapa...gharama ya dawa hiyo ilikuwa sh.18,000 yule mteja alishangaa kwani alikuwa akinunua katika duka la dawa binafsi sh. 48,000 hivyo aliona unafuu na umuhimu wa duka hili,"alisema.


Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli kwa hospitali za serikali za kanda na mikoa kuwa na duka la dawa la MSD. 

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando afungua rasmi duka la dawa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambalo linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando afungua rasmi duka la dawa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambalo linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
http://2.bp.blogspot.com/-In00xPgLWZg/Vl7t4tXFzuI/AAAAAAADbtQ/PClxwfsOKtg/s640/0013.JPG
http://2.bp.blogspot.com/-In00xPgLWZg/Vl7t4tXFzuI/AAAAAAADbtQ/PClxwfsOKtg/s72-c/0013.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/katibu-mkuu-wa-wizara-ya-afya-na-ustawi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/katibu-mkuu-wa-wizara-ya-afya-na-ustawi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago