Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue aendelea kuwasisitiza watumishi wa umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi

Katibu Mkuu Kiongozi  Mhe. Balozi Ombeni Sefue akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) beji yenye jina lake ambayo ame...


Katibu Mkuu Kiongozi  Mhe. Balozi Ombeni Sefue akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) beji yenye jina lake ambayo amewaagiza watumishi wa Umma kuivaa wanapokuwa  katika maeneo  yao ya  kazi. Balozi Sefue alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank.
---
Na Anna Nkinda – Maelezo
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa  katika maeneo  ya  kazi.

Mhe. Balozi Sefue aliutoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine. 

Alisema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza  watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao.
“Nimeamua kuonyesha mfano kwa vitendo kufuatia agizo nililolitoa kwa watumishi wa Umma kwa kuvaa beji inayonitambulisha jina langu , nilisema nitakuwa wa kwanza kuvaa jina langu nimevaa. Kama mtumishi wa umma atakuwa na mashaka ajue mimi nimeshalivaa”.

“Mtumishi wa umma anapomuhudumia mwananchi ni lazima ajue amehudumiwa na nani, mtumishi wa Umma akifanya  kazi zake kwa kutenda haki sidhani kama ataogopa kuvaa beji inayomtambulisha jina lake hivyo basi kama nilivyoagiza watumishi wote wa Umma mvae beji zinazowatambulisha majina yenu”, alisisitiza Mhe. Balozi Sefue.

Mhe. Balozi Sefue alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Sa
laam na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue aendelea kuwasisitiza watumishi wa umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue aendelea kuwasisitiza watumishi wa umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi
http://2.bp.blogspot.com/-e4dkCp3XctQ/Vl7z4UncIYI/AAAAAAADbvQ/kKpE_dMRA8o/s640/index2.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-e4dkCp3XctQ/Vl7z4UncIYI/AAAAAAADbvQ/kKpE_dMRA8o/s72-c/index2.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/katibu-mkuu-kiongozi-balozi-sefue.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/katibu-mkuu-kiongozi-balozi-sefue.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago