Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Kanusho Kali Kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Kuhusu upotoshwaji unaondelea katika mitandao ya kijamii hususan facebook, Instagram na WhatsApp ambapo sehemu ya upotoshaji huo imenukuliwa kama ifuatavyo “Wizara imetoa tamko kuwa kuanzia januari 2016 mavazi yote yasiyo stahiki ambayo hayaendani na mila na desturi zetu Wizara yangu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitafumbia macho mavazi hayo.

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo inap...

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo inapenda kuujulisha Umma kwamba kumekuwapo na upotoshwaji unaondelea katika mitandao ya kijamii hususan facebook, Instagram na WhatsApp ambapo sehemu ya upotoshaji huo imenukuliwa kama ifuatavyo “Wizara imetoa tamko kuwa kuanzia januari 2016 mavazi yote yasiyo stahiki ambayo hayaendani na mila na desturi zetu Wizara yangu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitafumbia macho mavazi hayo.

HAYARUHUSIWI KUVALIWA SEHEMU ZIFUATAZO
  1. Kwenye masoko makubwa
  2. Hospitali kubwa(Private or Public)
  3. Maofisini na Vyuoni
  4. Mijini kwenye mikusanyiko ya watu wengi
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa endapo kwa wale ambao watavaa mavazi haya ikiambatana na faini ya sh. 100,000/=” mwisho wa kunukuu.

Tunachukua fursa hii kukanusha vikali taarifa hizo kuwa siyo za kweli na kwamba mhusika amefanya uhalifu wa kimtandao kwa kuaanda taarifa yake ya uongo na kuibandika katika uso wa Tovuti ya Wizara yenye anuani: www.habari.go.tz kwa lengo la kuipotosha jamii.
Kufuatia uharifu huo Serikali inatoa onyo kali na haitawavumilia wale wote wanaokiuka misingi ya sheria ya mtandao ya mwaka 2015 ambayo inakataza kusambaza taarifa za uongo na haitasita kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote watakaobainika kufanya uharifu huo.

Pamoja na upotoshaji huo wa makusudi napenda pia kutumia wasaa huu kuwakumbusha watumishi wa umma na jamii yote kwa ujumla kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma inao Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 3 wa mwaka 2007 kuhusu mavazi kwa watumishi wa Umma. Waraka huo umeainisha mavazi ambayo hayafai kuvaliwa katika ofisi za umma kwa wanawake na wanaume; aidha umeelekeza aina za mitindo ya nywele isiyofaa pamoja na aina za viatu visivyofaa.

Mifano ya mavazi yasiyokubalika kwa watumishi wa umma wanawake ni kama vile nguo zinazobana, nguo fupi ambazo zinaacha magoti wazi, nguo ambazo zinaacha sehemu ya mwili wazi kama vile kitovu na kifua, nguo ambazo zina picha, michoro, na maandishi ambayo hayaendani na shughuli za Serikali, kaptura aina yoyote ile kama vile pedo na pensi, nguo zinazoonyesha maungo ya mwili (transparent), suruali za ‘Jeans’, na nguo zingine zote zenye kukinzana na maadili ya utumishi wa umma na jamii kwa ujumla.

Aidha, kwa upande wa wanaume mavazi yasiyokubalika ni pamoja na nguo ambazo ni za kazi maalum kama vile michezo (hizi zivaliwe wakati wa shughuli hiyo tu), nguo ambazo zina michoro, maandishi na picha ambazo haziendani na shughuli za Serikali, nguo zinazobana, kaptura ya aina yoyote, suruali yoyote inayoachwa bila kupindwa, suruali za “Jeans” na Fulana “T-shirts” (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika), Kikoi au msuli, nguo zenye maandishi ya chama chochote cha siasa na yenye kuonyesha ushabiki wa kitu fulani.

Pamoja na kuwepo kwa miongozo ya mavazi yanayostahili kwa watumishi wa umma, tafsiri ya mavazi ya heshima hutegemea mila na desturi ya jamii husika.
​ 
Imetolewa na 
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,​
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Kanusho Kali Kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Kuhusu upotoshwaji unaondelea katika mitandao ya kijamii hususan facebook, Instagram na WhatsApp ambapo sehemu ya upotoshaji huo imenukuliwa kama ifuatavyo “Wizara imetoa tamko kuwa kuanzia januari 2016 mavazi yote yasiyo stahiki ambayo hayaendani na mila na desturi zetu Wizara yangu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitafumbia macho mavazi hayo.
Kanusho Kali Kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Kuhusu upotoshwaji unaondelea katika mitandao ya kijamii hususan facebook, Instagram na WhatsApp ambapo sehemu ya upotoshaji huo imenukuliwa kama ifuatavyo “Wizara imetoa tamko kuwa kuanzia januari 2016 mavazi yote yasiyo stahiki ambayo hayaendani na mila na desturi zetu Wizara yangu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitafumbia macho mavazi hayo.
http://3.bp.blogspot.com/-BPnE_2sTDOg/VoEZ-M3Lf2I/AAAAAAADc98/pWPUyU-jc_Q/s200/Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
http://3.bp.blogspot.com/-BPnE_2sTDOg/VoEZ-M3Lf2I/AAAAAAADc98/pWPUyU-jc_Q/s72-c/Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/kanusho-kali-kutoka-wizara-ya-habari.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/kanusho-kali-kutoka-wizara-ya-habari.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago