Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

JAPAN YAIPATIA TANZANIA TSH. BILIONI 210 KUENDELEA MRADI WA UMEME TANZANIA NA KENYA

 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile na Balozi wa Japani nchini Bw.Masaharu Yoshida wakisaini mkataba wa mkopo. Nyuma y...

 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile na Balozi wa Japani nchini Bw.Masaharu Yoshida wakisaini mkataba wa mkopo. Nyuma yao kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Omar Chambo, kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Seiji Kihara wakishuhudia tukio hilo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Jijini Dares Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile na Balozi wa Japani nchini Bw. Masaharu Yoshida wakibadilishana hati ya mkataba wa mkopo wa Shilingi Bilioni 210 kwa ajili ya mradi wa Umeme kati ya Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi wa matumizi ya mkopo wa bilioni 210 baada ya kusaini mkataba wa mkopo huo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.
--
 
 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mkataba na Serikali ya Japani kiasi cha shilingi Bilioni 210 kwa ajili ya maendeleo ya mradi wa njia ya kusafirishia umeme kati ya Tanzania na Kenya ambao utasaidia upatikanaji wa umeme wa kutosha.

Mkataba huo wa masharti nafuu ulisaininiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida jijini Dar es Salaam.

Akizungumza  na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba huo Dkt. Likwelile alisema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika kusambaza nyaya za umeme zenye  KV400, na urefu wa kilometa 414.5 kati ya Singida na Namanga kupitia Babati na Arusha.

Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutachochea maendeleo ya jamii na  uchumi nchini kwa kuleta muungano wa kibiashara katika nchi za Afrika Mashariki.

Naye Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida alisema kuwa mkopo huo utafanikisha kusambaza nyanya za umeme zenye urefu wa takribani kilometa 508 kati ya Tanzania na Kenya ambapo Tanzania itasambaza kilometa 415 wakati Kenya itakuwa na kilometa 93.

Japani imekuwa ikisaidia Tanzania katika miradi ya umeme kwa muda mrefu, miradi ambayo tayari imekamilika ni pamoja na usambazaji umeme Zanzibar, mradi wa usambazaji nyaya za umeme mkoani Kilimanjaro na mradi wa kutengeneza nyaya mpya za umeme  jijini Dar es Saalam.


IMETOLEWA NA 
WIZARA YA FEDHA
KITENGO CHA MAWASILIANO

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: JAPAN YAIPATIA TANZANIA TSH. BILIONI 210 KUENDELEA MRADI WA UMEME TANZANIA NA KENYA
JAPAN YAIPATIA TANZANIA TSH. BILIONI 210 KUENDELEA MRADI WA UMEME TANZANIA NA KENYA
http://4.bp.blogspot.com/-PZkyn3NKf8k/VnF2xCt3Y1I/AAAAAAADchM/zdSzt-lp-6g/s640/fd2.jpg
http://4.bp.blogspot.com/-PZkyn3NKf8k/VnF2xCt3Y1I/AAAAAAADchM/zdSzt-lp-6g/s72-c/fd2.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/japan-yaipatia-tanzania-tsh-bilioni-210.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/japan-yaipatia-tanzania-tsh-bilioni-210.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago