Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Benki ya ADB yatoa mkopo wa bilioni 750 kwa Tanzania kwa ajili miradi miwili ya maendeleo

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akisaini mkataba kutoka Benki ya Maendeleo Afrika kwa ajili ya Mradi w...

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akisaini mkataba kutoka Benki ya Maendeleo Afrika kwa ajili ya Mradi wa Ujenzi ,kulia ni mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero akitia saini wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akikabidhiana hati ya makubaliano ya msaada wa fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi na mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa makabidhiano ya fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi kulia akiwa na mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale akiongea na waandishi wa habari baada ya makabidhiano ya fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.PICHA ZOTE NA ALLY DAUD- MAELEZO
---
Na jacquline Mrisho-maelezo Dsm
Wizara ya Fedha na Benki ya Maendeleo Afrika(ADB) zimesaini mikataba yakuikopesha Tanzania shilingi bilioni 750 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi sekta mbili za maendeleo ya ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege nchini.

Mikataba hiyo imesainiwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt Servacius Likwelile kwa upande wa Tanzania na Mwakilishi wa Benki hiyo Dkt Tonia Kandiero.
Akizungumza mara baada ya kusaini mikataba hiyo Dkt . Likwelile alisema kuwa katika mkopo wa kwanza utasaidia katika kuinua uchumi nchini kwa kuimarisha miundo mbinu ya barabara ya Tanzania bara na visiwani.

Dkt Servacius Likwelile aliongeza kuwa,mradi huu utapunguza gharama za matengenezo ya barabara pamoja na muda usafirishaji na ukarabati wa vyombo vya usafirishaji.

Naye Mwakilishi wa Benki Maendeleo ya Afrika Dkt Tonia Kandiero alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara kwa ajili ya kuimarisha kilimo hasa katika mikoa ya Tabora, Katavi na Ruvuma ambapo asilimia 90 ya watu wake ni wakulima.

Maeneo ambayo mradi huu yatakayoshughulika ni barabara ya kutoka Tabora (Pangale) hadi Mpanda na nyingine kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay kwa Tanzania Bara na kwa Zanzibar barabara itatoka Bububu hadi Mkokotoni na nyingine kutoka vijijini hadi Bitumen standadi.Mkopo mwingine unaelekezwa katika ujenzi wa viwanja vya ndege vya Msalato kwa Tanzania Bara na Pemba kwa Zanzibar.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Benki ya ADB yatoa mkopo wa bilioni 750 kwa Tanzania kwa ajili miradi miwili ya maendeleo
Benki ya ADB yatoa mkopo wa bilioni 750 kwa Tanzania kwa ajili miradi miwili ya maendeleo
http://1.bp.blogspot.com/-sUPLEGSLDJw/VmGURFsRwMI/AAAAAAADb3Y/O0hIzVjj61I/s640/LI1.jpg
http://1.bp.blogspot.com/-sUPLEGSLDJw/VmGURFsRwMI/AAAAAAADb3Y/O0hIzVjj61I/s72-c/LI1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/benki-ya-adb-yatoa-mkopo-wa-bilioni-750.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/benki-ya-adb-yatoa-mkopo-wa-bilioni-750.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago