Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

BELLA KUFUNGA MWAKA NA KOFFI, DAR LIVE

KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’. Na Mwandishi Wetu KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa ku...

BELAKING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’.
Na Mwandishi Wetu KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kufunga mwaka (Desemba 31) na wimbo alioufanya na mkongwe wa muziki kutoka Kongo (DRC), Koffi Olomide uitwao Acha Kabisa, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. Akizungumza na mtandao huu, Bella anayetamba na Wimbo wa Nashindwa alisema usiku huo mashabiki watafunga mwaka kwa kuimba na kucheza ngoma zake zote kali kama vile Nani Kama Mama, Nakuhitaji, Msaliti, Nashindwa, Amerudi na nyingine kibao. “Usiku huo nitafunga mwaka na kufungua mwaka mwingine nikiwa na bendi yangu ya Malaika Music huku tukitoa sapraiz kwa mashabiki wetu wote, pia kwa mara ya kwanza nitawaonjesha Wimbo wa Acha Kabisa niliofanya na Koffi Olomide pamoja na kutambulisha wimbo wangu mpya mwingine,” alisema Bella. Mashabiki pia wategemee kupata sebene la aina yake kutoka kwa Malaika itakayokuwa na vichwa kama Adaya, Petit Mauzo, Pilu, Mico Bella, Chesco Vuvuzela, Yanick Soslo, Babu Bomba, Kadogoo Machine na wengine wengine wengi. 5_5 
Baada ya kufunga mwaka, katika Sikukuu ya Mwaka Mpya (Januari 1), bendi kongwe ya muziki wa Dansi, The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ikiongozwa na Ali Chocky itakuwa na kazi moja ya kulishambulia jukwaa kwa kutoa sebene la kisasa. Akizungumzia shoo ya kufungua mwaka, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa siku hiyo pazia la burudani litafunguliwa mapema kuanzia asubuhi kwa kutoa nafasi kwa watoto wote kusherehekea kuukaribisha mwaka mpya. “Tutakuwa na kundi linalotikisa kunako miondoko ya sarakasi na mazingaombwe kwa watoto la Masai Warriors ambapo watatoa burudani zote bila kusahau watoto wote wataburudika na michezo mingi kama vile kuogelea, kuteleza, kubembea pamoja na kucheza ndani ya ndege maalum,” alisema Mbizo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: BELLA KUFUNGA MWAKA NA KOFFI, DAR LIVE
BELLA KUFUNGA MWAKA NA KOFFI, DAR LIVE
http://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2015/12/BELA.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/bella-kufunga-mwaka-na-koffi-dar-live.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/bella-kufunga-mwaka-na-koffi-dar-live.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago