Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

BALOZI WILSON MASILINGI AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VYAMA VYA SIASA DMV AHUDHURIA MKUTANO WA HALMASHAURI YA CCM DMV

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson's Masilingi leo Jumamosi Desemba 5, 2015 alihudhuria mkutano w...


Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson's Masilingi leo Jumamosi Desemba 5, 2015 alihudhuria mkutano wa Halmashauri ya CCM tawi la DMV ikiwa ni moja ya ziara zake anazotarajiwa kuzifanya kutembelea matawi ya vyama vya siasa nchiMarekani yenye lengo la kudumisha mshikamano na ushirikiano wa Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao.

Akiongea kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV Mhe. Wilson Masilingi amesema lengo kuu ni kuwa karibu na vyama vya siasa kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano ndani ya Jumuiya za Watanzania nchini Marekani na pia kuvitambua kama sehemu na sura ya Diaspora na kutoa wito kwa Watanzania waishio Marekani kuelekeza nguvu katika kuwekeza nyumbani bila kujali ufuasi wa chama unachoamini au kushabikia, wote ni Watanzania.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliiomba Halmashauri hiyo ya CCM DMV kusaidia katika maendeleo ya Tanzania kwa kupanua wigo wao pamoja na kwamba lengo lao ni siasa na siasa ni sehemu ya maisha ya jamii na maendeleo ya jamii yanategemea siasa, kwa hiyo basi mnaposikia kuna muwekezaji yupo tayari kuwekeza Tanzania msisite Ubalozi upo wazi na utafanya kila liwezekanalo kuhakikisha muwekezaji huyo hapati vikwazo vyovyote.

Mwisho Balozi Wilson Masilingi aliwashukuru Watanzania kwa kuwa mabalozi wazuri nchini Marekani na kuwaasa kuishi kwa kufuata misingi na sheria za nchi ya Marekani.

 Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea jambo na mwenyekiti wa tawi CCM DMV Bwn. George Sebo kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 mkutano uliofanyika Hampton Inn, College Park, Maryland. Picha na Kwanza Production/Vijimambo Blog
Mkutano ulianza kwa sala na kuwakumbuka wote waliotangulia mbele ya haki.

Mwenyekiti tawi la CCM DMV Bwn. George Sebo akifungua kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College Park, Maryland.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea machache kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College Park, Maryland.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea machache kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM DMV

Picha ya pamoja.
Bwn. John Mbatta katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Given  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Catherine  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Tino Malinda  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Aunty Grace Sebo  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Grace Mlingi  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Mzee Joel  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Dr. Secelela Malecela  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Katibu wa CCM DMV Bi.Jesca Mushala  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.
Mwenyekiti wa CCM DMV Bwn. George Sebo  katika picha ya pamoja na Balozi Wilson Masilingi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: BALOZI WILSON MASILINGI AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VYAMA VYA SIASA DMV AHUDHURIA MKUTANO WA HALMASHAURI YA CCM DMV
BALOZI WILSON MASILINGI AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VYAMA VYA SIASA DMV AHUDHURIA MKUTANO WA HALMASHAURI YA CCM DMV
http://1.bp.blogspot.com/-2_pIUofw3qE/VmNiOvz717I/AAAAAAAEHhI/44QPrWTMu14/s640/IMG_2610%2B%25282%2529.JPG
http://1.bp.blogspot.com/-2_pIUofw3qE/VmNiOvz717I/AAAAAAAEHhI/44QPrWTMu14/s72-c/IMG_2610%2B%25282%2529.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/12/balozi-wilson-masilingi-aanza-ziara-ya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/12/balozi-wilson-masilingi-aanza-ziara-ya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago