Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Zijue saa 72 za Rais Dk John Magufuli akiwa Ikulu

Rais Dr John Magufuli --- By Waandishi Wetu, Mwananchi Dar/Mikoani. Baada ya Rais John Magufuli kuanza kwa kishindo maish...

Rais Dr John Magufuli
---
By Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar/Mikoani. Baada ya Rais John Magufuli kuanza kwa kishindo maisha ya Ikulu kwa kutekeleza kauli mbiu yake ya “hapa kazi tu”, watu walioongea na gazeti hili wameonyesha kuridhishwa, lakini baadhi wakimpinga na wengine kumkosoa.

Akiwa kwenye kampeni za kuutaka urais kwa tiketi ya CCM, alisema ataanza kazi mara baada ya kuapishwa, na atafanya kazi usiku na mchana.


Katika siku nne za kwanza, Rais huyo wa Serikali ya Awamu ya Tano pia ametoa maagizo kadhaa, ikiwemo kuitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuhakikisha inakusanya kodi hasa kwa kuwabana wafanyabiashara wakubwa, kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kutangaza elimu bure kuanzia mwakani.
Rais Magufuli alitoa agizo hilo baada ya kufanya kikao na makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade kwa lengo la kutoa mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Alisema mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nchi huko nje, ndiyo watakaotakiwa kufanya shughuli zote kwenye nchi wanazofanya kazi hadi hapo atakapolitolea suala hilo uamuzi mwingine.

Wasemavyo wasomi
Wengi waliozungumza na gazeti hili walimsifu Rais Magufuli kutokana na kuagiza walipa kodi, hasa wafanyabiashara wakubwa wadhibitiwe, kusimamisha safari za nje, wakisema fedha zitakazookolewa zitasaidia katika kutekeleza ahadi ambazo yeye na chama chake walizitoa wakati wa kampeni.

“Ingawa kitaalamu huwezi kupima utendaji kwa siku tatu, Rais Magufuli ameanza kazi kwa kutoa maagizo ili kuhakikisha anatekeleza aliyoahidi kama kutoa elimu bure ya msingi hadi sekondari,” alisema Profesa Lugano Kusiluka wa Chuo Kikuu Huria (OUT).“Sasa ni wajibu wa watendaji wa serikali kutekeleza.”Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea......

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Zijue saa 72 za Rais Dk John Magufuli akiwa Ikulu
Zijue saa 72 za Rais Dk John Magufuli akiwa Ikulu
http://1.bp.blogspot.com/-VV0Iee-iwaw/VkCcmNn6-WI/AAAAAAADauw/ynQxCePXkKI/s640/john-magufuli.jpg
http://1.bp.blogspot.com/-VV0Iee-iwaw/VkCcmNn6-WI/AAAAAAADauw/ynQxCePXkKI/s72-c/john-magufuli.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/11/zijue-saa-72-za-rais-dk-john-magufuli.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/11/zijue-saa-72-za-rais-dk-john-magufuli.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago