Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

VIDEO NA TAARIFA RASMI:BODI YA MIKOPO YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016 BODI  y...


BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016

BODI  ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuutaarifu umma kuwa kuna taarifa zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi haitatoa mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka wa masomo 2015/2016. Taarifa hizo si za kweli na hivyo Bodi inauomba umma kuzipuuza. 

Aidha, Bodi ya Mikopo inapenda kutoa taarifa kwamba hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 40,836 wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo na katika Awamu ya Pili iliyotolewa tarehe 9 Novemba, 2015 jumla ya waombaji 28,554 wamepangiwa mikopo.

Majina ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.

Lengo la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016, ambao ni 50,830, wanapata mikopo.

Aidha, Bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa unaendelea.

         
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: VIDEO NA TAARIFA RASMI:BODI YA MIKOPO YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
VIDEO NA TAARIFA RASMI:BODI YA MIKOPO YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
https://i.ytimg.com/vi/D98xDcSCGks/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/D98xDcSCGks/default.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/11/video-na-taarifa-rasmibodi-ya-mikopo.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/11/video-na-taarifa-rasmibodi-ya-mikopo.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago