Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

UJUMBE WA MKURUGENZI MKUU WA UNESCO KUHUSIANA NA SIKU YA SAYANSI YA DUNIANI

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova. -- Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Lenye makao ...


science
Irina_Bokova1
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova.
--
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Lenye makao yake makuu jijini Paris, Ufaransa kupitia Mkurugenzi wake Mkuu limetoa ripoti ya ujumbe wake kuelekea siku ya Sayansi Duniani kwa amani inayotarajia kuadhimishwa leo hii Novemba 10, Duniani kote.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO , Bi Irina Bokova, katika ujumbe wake, juu ya maadhimisho ya leo ameweza kugusia mambo mbalimbali:

"Hii Siku ya Sayansi Duniani kwa Amani na Maendeleo imekuja miezi miwili baada ya makubaliano ya Agenda 2030 ya maendeleo endelevu.
Ajenda hii mpya inajumuisha maono mapya kwa binadamu, kwa dunia, kwa amani , kwa miaka 15 ijayo na sayansi inasimamia katika moyo wake kama kichocheo cha mageuzi chanya na maendeleo.

Serikali zote kwa ujumla zinatambua leo nguvu ya sayansi ya kutoa majibu muhimu kwa usimamizi mzuri wa maji, kwa ajili ya hifadhi na matumizi endelevu ya bahari, ulinzi wa mazingira na viumbe hai, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na majanga, na kuendeleza uvumbuzi na kuondokana umaskini na kupunguza tofauti .

Kufanya haya, tunahitaji kuelewa wazi zaidi mazingira ya kimataifa ya sayansi na tunahitaji zana bora kufuatilia maendeleo .
Tutazindua toleo jipya katika Siku ya Sayansi Duniani kwa ajili Amani na Maendeleo 2015, kuonyesha mwelekeo wa sayansi, teknolojia na maendeleo kwa kila nchi katika ngazi zote za maendeleo. Kuongezeka kwa wasiwasi wa ukame, mafuriko, vimbunga na matukio mengine ya asili yamesababisha Serikali kupitisha mikakati katika ngazi za kitaifa na kikanda kulinda kilimo, kupunguza hatari ya maafa na kuongeza vyanzo vya kitaifa vya nishati.


Kuongezeka kwa uwekezaji katika sayansi huonyesha kutambuliwa zaidi haja ya kujenga jamii na uchumi wa kijani, kuleta mabadiliko katika sera na sheria ikiwa ni pamoja na maadili na tabia.

Maswali haya yatashughulikiwa katika mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi ( COP21 ) utakaofanyika Paris mwezi ujao, wakati viongozi kutoka pande zote za dunia watakapokusanyika kupitisha mkataba mpya wa ushirikiano wa kimataifa wa kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

Sayansi, teknolojia na ubunifu ni muhimu hapa, na ni lazima tufanye kila kitu kusaidia jamii zote duniani, kujenga na kubadilishana maarifa. Agenda ya 2030, pamoja na ajenda ya maamuzi ya Addis Ababa, imetoa wito kujenga sera imara za kitaifa za sayansi, teknolojia na ubunifu pamoja na mifumo, ili kuwezesha uhamishaji wa teknolojia na ubunifu, ambayo UNESCO imejizatiti kamilifu .

Huu ni ujumbe wa Ripoti ya Sayansi ya UNESCO na hii Siku ya Sayansi Duniani kwa Amani na Maendeleo. Nawakaribisha wote kujiunga na sisi katika kuuchukua huu ujumbe duniani kote na kujenga maisha bora ya baadaye kwa wote " Alimalizia Mkurugenzi Mkuu huyo.
Kwa habari zaidi ya ripoti hii inapatikana katika tovuti ya UNESCO ; www.unesco.org
Kwa maelezo zaidi unaweza pia kuwasiliana na Ofisi ya UNESCO iliyopo karibu nawe, na kwa Dar es Salaam kupitia: barua pepe: dar-es-salaam@unesco.org au tovuti: www.unescodar.or.tz na mawasiliano ya ofisi Simu ya Ofisi: +255 22 2915400

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: UJUMBE WA MKURUGENZI MKUU WA UNESCO KUHUSIANA NA SIKU YA SAYANSI YA DUNIANI
UJUMBE WA MKURUGENZI MKUU WA UNESCO KUHUSIANA NA SIKU YA SAYANSI YA DUNIANI
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/11/science.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/11/ujumbe-wa-mkurugenzi-mkuu-wa-unesco.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/11/ujumbe-wa-mkurugenzi-mkuu-wa-unesco.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago