Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Serikali ya awamu ya tano imepanga kutumia takribani shilingi bilioni 6 kununua kivuko kipya.

Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet ...

Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle (wa pili kutoka kulia) akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Dar es Salaam kuhusu mikakati ya Serikali kuboresha huduma za vivuko nchini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa, kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi na Umeme kutoka Wizara ya Ujenzi Dkt. William Nshama na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Segolena Francis.
Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Dar es Salaam kuhusu mpango wa Serikali kununua kivuko kipya kwa ajili ya wakazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa watendaji wa Wizara ya Ujenzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
--  
Na Frank Mvungi.
Serikali ya awamu ya tano imepanga kutumia takribani shilingi bilioni 6 kununua kivuko kipya kitakachotumika kutoa huduma kwa  wananchi katika eneo la feri hadi kigamboni Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko  kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle  amesema ununuzi huo umelenga kuboresha huduma za usafiri wa vivuko kote nchini.

Akizungumzia uwezo wa kivuko kitakachonunuliwa kwa ajili ya jiji la Dar es salaam  Maselle amesema kuwa kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 170 na kitakuwa na injini 4 hali itakayoongeza tija katika kuwahudumia wananchi.


“Serikali imepanga kununua vivuko vitatu (3) vipya  ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuondoa kabisa tatizo la vivuko hapa nchini ”alisisitiza Maselle”


Akizungumzia mwenendo wa vivuko hapa nchini Maselle amesema kuwa viko katika hali nzuri na mpango wa Serikali kwa sasa ni kuvifanyia matengenezo ya mara  kwa mara ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma yenye ubora unaotakiwa.


Pia Masele amebainisha kuwa Serikali itatumia zaidi ya bilioni 3 kujenga kivuko kipya cha Pangani ambapo kazi ya ujenzi wake itaanza wakati wowote kwa kuwa taratibu zote za maandalizi zimeshakamilika.


Kwa upande wa utoaji wa Taarifa kwa wananchi kuhusu hali ya vivuko hapa nchini Maselle anabainisha kuwa wamejipanga kuwapa wananchi taarifa  kwa wakati  kulingana na hali ya vivuko na hatua zinazochukuliwa ikiwemo kufanya ukarabati ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.

Akizungumzia Idadi ya vivuko vinavyosimamiwa na TEMESA  inasimamia na kuendesha vivuko vyote vya Serikali nchini ambapo kwa Sasa kuna jumla ya Vivuko 28 vinavyofanya kazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

TEMESA  ilianzishwa kwa sheria ya wakala Na. 3 ya mwaka 1997 ambayo inalenga katika utekelezaji wa Serikali wa kuboresha huduma kwa umma katika Wizara za Serikali na Taasisi zake. TEMESA Ilianza rasmi mwezi Juni 2006 baada ya tangazo la Serikali Na. 254 La tarehe 26/08/2005 ambapo Wakala huo unatoa huduma katika Nyanja za Uhandisi Mitambo,Umeme,Electroniki na uendeshaji wa  Vivuko.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Serikali ya awamu ya tano imepanga kutumia takribani shilingi bilioni 6 kununua kivuko kipya.
Serikali ya awamu ya tano imepanga kutumia takribani shilingi bilioni 6 kununua kivuko kipya.
http://3.bp.blogspot.com/-rKwxZdihWWU/VlRuMzmlpBI/AAAAAAADbdE/1rXCrJWxgxg/s640/01.JPG
http://3.bp.blogspot.com/-rKwxZdihWWU/VlRuMzmlpBI/AAAAAAADbdE/1rXCrJWxgxg/s72-c/01.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/11/serikali-ya-awamu-ya-tano-imepanga.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/11/serikali-ya-awamu-ya-tano-imepanga.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago