Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Raia wanne kutoka China,walipandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya kujibu mashtaka matatu ya uhujumu uchumi likiwamo la kukutwa na pembe kumi na moja za faru zenye thamani ya Sh 902.8milioni.

Raia wa China wakiingia katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Mbeya jana wakikabiliwa na mashtaka matatu wakituhumiwa k...

Raia wa China wakiingia katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Mbeya jana wakikabiliwa na mashtaka matatu wakituhumiwa kukamatwa na nyara za Serikali ambazo ni pembe 11 za Faru. Picha na Godfrey Kahango   
---


By Godfrey Kahango, Mwananchi
Raia wanne kutoka China, jana walipandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya kujibu mashtaka matatu ya uhujumu uchumi likiwamo la kukutwa na pembe kumi na moja za faru zenye thamani ya Sh 902.8milioni.

Washtakiwa hao ni pamoja na Song Leo (33), Xiao Shaodan (29), Chen Jianlin (34) na Hu Liang (30).
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa akisaidiana na Simon Wankyo, alidai kuwa washtakiwa wote kwa pamoja walishiriki kuhujumu uchumi kinyume cha sheria ya nchi.

Pia, alidai kuwa walipanga njama na kutekeleza kuingiza nchini pembe hizo za faru bila kibali cha Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa, kwa kumiliki nyara hizo bila kibali.

Mulisa alidai kuwa washtakiwa walikamatwa Novemba 6, mwaka huu katika mpaka wa Kasumulu wilayani Kyela wakiwa wamezificha pembe hizo kwenye gari walilokuwa wakisafiria kutoka nchini Malawi kuja Tanzania.

Hata hivyo, washtakiwa wote walikana mashtaka na Wakili Mulisa alisema upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Alimuomba Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa, Michael Mteite apange tarehe ya kuendelea kusikilizwa kesi hiyo.

Wakili wa upande wa utetezi, Ladslaus Lwekaza aliiomba mahakama iwapatie dhamana wateja wake kwa madai kwamba mashtaka wanayokabiliwa nayo yanatoa fursa ya kuwapo kwa dhamana hiyo. Hoja hiyo ilipingwa na mawakili wa Jamhuri, waliodai kuwa Mkurugenzi wa mashtaka amezuia dhamana.

Mteite alikubaliana na hoja ya upande wa mashtaka ya kuzuia dhamana kwa washtakiwa hao na aliamuru warudishwe mahabusu. Kesi hiyo itaendelea leo na itasikilizwa kwa mfululizo siku mbili.     


COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Raia wanne kutoka China,walipandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya kujibu mashtaka matatu ya uhujumu uchumi likiwamo la kukutwa na pembe kumi na moja za faru zenye thamani ya Sh 902.8milioni.
Raia wanne kutoka China,walipandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya kujibu mashtaka matatu ya uhujumu uchumi likiwamo la kukutwa na pembe kumi na moja za faru zenye thamani ya Sh 902.8milioni.
http://1.bp.blogspot.com/-dDArw5fywFA/VlXCiFnymXI/AAAAAAADbeI/OI-1Sk7SKQc/s640/WachinaPHOTO.jpg
http://1.bp.blogspot.com/-dDArw5fywFA/VlXCiFnymXI/AAAAAAADbeI/OI-1Sk7SKQc/s72-c/WachinaPHOTO.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/11/raia-wanne-kutoka-chinawalipandishwa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/11/raia-wanne-kutoka-chinawalipandishwa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago