Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

PICHA NA TAARIFA:ZIRA YA KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR LEO,ATEMBELEA MASHINE YA MRI,ST-SCAN NA JENGO LA TAASISI YA MIFUPA YA MOI

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni jambo katika mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika leo k...

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni jambo katika mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba wagonjwa hawapaswi kulala chini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete baada ya kufuatilia agizo la Rais John Pombe Magufuli ambaye awali aliagiza wagonjwa wasilale chini. Rais Magufili aliitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hivi karibuni na kutoa agizo hilo. Leo Balozi Sefue ameitembelea mashine ya MRI, ST-Scan na Jengo la Taasisi ya Mifupa ya MOI. Akiwa katika ofisi ambako ipo mashine ya MRI na ST-Scan Balozi Sefue amepewa taarifa ya matengenezo ya mashine hizo.
 Mmoja wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji wa mashine hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Jumatano.
 Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa mashine ya MRI kwa wakati baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo imehifadhiwa. Ofisa anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na kutekeleza wagonjwa kutolala chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye vitanda na siyo chini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi na Jamii, Dk Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, Othuman Wanin Kiloloma.Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
--
Katibu  Mkuu  Kiongozi  Balozi Ombeni  Sefue leo amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema  amekagua mashine za MRI na CT-SCAN  na kueleza kuwa spea zimeshafika na kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea. Pia amesema kwamba Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.
Pia,  amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za serikali.
Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali, Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia mifumo ya Tehama  na kuwa na maduka yao ya ndani.
Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando  na  watendaji wa MNH  ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.
Mwisho.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: PICHA NA TAARIFA:ZIRA YA KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR LEO,ATEMBELEA MASHINE YA MRI,ST-SCAN NA JENGO LA TAASISI YA MIFUPA YA MOI
PICHA NA TAARIFA:ZIRA YA KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR LEO,ATEMBELEA MASHINE YA MRI,ST-SCAN NA JENGO LA TAASISI YA MIFUPA YA MOI
http://2.bp.blogspot.com/-mQv56okUcfI/VlMYnSnLIAI/AAAAAAADbZA/9beGImw92Os/s640/002.JPG
http://2.bp.blogspot.com/-mQv56okUcfI/VlMYnSnLIAI/AAAAAAADbZA/9beGImw92Os/s72-c/002.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/11/picha-rasmizira-ya-katibu-mkuu-kiongozi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/11/picha-rasmizira-ya-katibu-mkuu-kiongozi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago