Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu (kushoto) akiwaongoza watendaji wakuu na maafisa wa jeshi hilo kuim...
Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP),
Ernest Mangu (kushoto) akiwaongoza watendaji wakuu na maafisa wa jeshi
hilo kuimba wimbo wa maadili wa jeshi hilo wakati wa ziara ya Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (wapili
kushoto). Ziara hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar
es Salaam leo, ilikuwa na lengo la kujitambulisha na kufahamiana na
watendaji hao. Watatu kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki,
wapili kulia ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi Clodwig
Mtweve, na kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamishna Suleiman Kova.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, John Mngodo, akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Polisi, wakati
wa mkutano wa Kujitambulisha na kufahamiana na Watendaji wakuu na Maafisa
wa Jeshi la Polisi uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar
es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mngodo alilipongeza jeshi hilo kwa
kusimamia Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu. Kulia kwa Katibu Mkuu
ni Inspekta Jenerali wa Jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu.
Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP),
Ernest Mangu (kushoto) akitoa taarifa ya Jeshi hilo wakati wa Ziara
ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo,
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam kwa lengo
la kujitambulisha na kufahamiana na watendaji wa jeshi hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, John Mngodo ( watano kulia), Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi
nchini (IGP), Ernest Mangu (watano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja
na Watendaji wakuu na Maafisa wa jeshi hilo muda mfupi baada ya kumaliza
ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, John Mngodo (kulia), akiagana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum
ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova baada ya kumaliza ziara yake
katika Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna
wa Lojistiki na Fedha wa jeshi hilo, Clodwig Mtweve, wapili kushoto
ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Musa Ali Musa, akifuatiwa na Mkurugenzi
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Diwani Athumani. Picha zote na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.