Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MKUTANO WA WABUNGE WA CCM WAMPITISHA MBUNGE WA KONGWA-CCM JOB NDUGAI KUWA MGOMBEA PEKEE WA NAFASI YA USPIKA

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari mara baada ya Wabunge wa CCM kupitisha jisha la Spika. ...

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari mara baada ya Wabunge wa CCM kupitisha jisha la Spika.

Katibu wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mbunge wa Mtama, Nape Nnauye alisema “Kamati ya Wabunge wote wa CCM imekamilisha kazi yake ya kwanza kuchambua na kupitisha moja kati ya majina matatu yaliyoteuliwa na Kamati Kuu.

“Kama tulivyoona wagombea wawili walijitoa, hivyo Job Ndugai
amepitishwa kwa kauli moja kugombea nafasi ya uspika. Tunamuombea kura kwa
sababu sifa zote anazo, bila shaka hakutatokea mgombea wa upinzani atakayezidi
sifa zake,” alisema Nape.
 Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC baada ya jina lake kupitishwa na wabunge wa CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM akipokea pongezi alizopewa na wabunge wa CCM kwa kazi nzuri iliyowapa CCM ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika oktoba 2015.
 Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC baada ya jina lake kupitishwa na wabunge wa CCM.

KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ndugu ABDULRAHMAN KINANA amefungua kikao cha kamati  ya wabunge wa CCM huku akiwahimiza wabunge hao kufanya kazi ili kutekeleza kauli mbiu ya rais dr JOHN MAGUFULI ya hapa kazi tu.
 
Akifungua kikao hicho leo mjini Dodoma ndugu KINANA amesema ili kuendana na kauli mbiu hiyo nilazima wabunge wote wafanye kazi. 
 
Amesema kazi waliyonayo kwa sasa ni kuwazungukia watanzania ambao wamewaamini kwa kuwa njia pekee ya kutafsiri imani hiyo ni kuwatumikia kwa nguvu zote.
 
Ndugu KINANA amewapongeza wabunge hao kwa kutafuta kura nyingi za rais juhudi ambayo imekiletea chama heshima kubwa na kuwahakikishia kuwa ofisi yake itaandaa siku maalum kabla ya bunge linalofuata ili kuwapa majukumu ya namna ya kuwatumikia wananchi.
 
Amesema kazi kubwa kwa wanasiasa ni kutekeleza ilani ya uchaguzi waliyonayo kazi ambayo ana imani kuwa wabunge hao wataitekeleza ipasavyo.
 
Awali akimkaribisha katibu mkuu,katibu wa wabunge wa CCM mama JENISTA MUHAGAMA amesema kikao hicho nimaalum kwa ajili ya kuchagua jina moja la atakayegombea nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Tanzania kutoka
katika majina matatu yaliyopitishwa na kamati kuu ya halmashauri ya CCM jana.
 
Majina hayo yaliyopitishwa ni la naibu spika mstaafu JOB NDUGAI,mbunge wa Afrika Mashariki ABDULLAH ALLY MWINYI na naibu mwanasheria mkuu wa serikali TULIA ACKSON MWASANSU ambaye ameteuliwa na rais kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya Tanzania.
 
Uchaguzi huo unasimamiwa na  wajumbe wa kamati kuu ya CCM ambao ndugu WILLIAM LUKUVI,MAUA DAFTARI na JERRY SILAA ambapo jina moja litakalopatikana litapelekwa kesho bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge wote.
 
SHUKRANI CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewashukuru watanzania kwa imani kubwa waliyoionyesha  katika uchaguzi mkuu uliopita uliowezesha kuwapa ushindi wabunge wa chama hicho kwa asilimia 74.8.
 
Akifungua kikao cha kamati cha wabunge wa CCM kilichofanyika ukumbi wa white house mjini Dodoma katibu mkuu wa chama hicho ndugu ABDULRAHMAN KINANA amesema kitendo hicho kimedhihirisha imani kubwa waliyonayo watanzania kwa CCM.
 
Amesema watanzania wametafsiri imani kwa kukipa kura CCM na kusema katika majimbo tisa yanayofanya uchaguzi
mdogo tayari CCM imeshinda katika jimbo la Lulindi lililopo mkoani Tanga.
Aidha amesema katika kata 14 zilizofanya uchaguzi mdogo katika jimbo hilo CCM imepata kata 10 na upinzani kata 4. 
 Wajumbe wa Kamati Kuu wakiwa katika mkutano huo.

 Mbunge mteule wa Bumbuli-ccm january makamba akifurahia jambo kala ya kuanza kwa mkutano maalum wa wabunge wa chama hicho wa kuteua jina la Mgombea Uspika kupitia CCM uliofanyika leo Jumatatu Novemba 16, 2015 katika makao makuu ya Chama hicho mjini Dodoma.
 Mbunge Mteule wa Nzega mjini Hussein Bashe akizungumza na Mbunge mteule wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye pamoja na Jerry Slaa (katikati) kabla ya zoezi la upigaji kura kwenye ukumbi wa NEC.
 Wabunge Wateule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Mhe. Sophia Simba (Viti Maalum) wakibadilishana mawazo katika ukumbi wa makao ya chama hicho mjini Dodoma leo Jumatatu Novemba 16, 2016 katika mkutano maalum wa wabunge wa chama hicho wa kuteua jina la Mgombea Uspika kupitia CCM wakati wa mkutano maalum wa wabunge wa chama hicho wa kuteua jina la Mgombea Uspika kupitia CCM.
Masanduku yaliyotumiwa na Wabunge Wateule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupiga kura kumpitisha mgombea Uspika kupitia CCM Job Ndugai 
 Wabunge Wateule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (Musoma Vijijini) naMhe. John Mpata (Nkasi Kusini) wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa mkutano maalum wa wabunge wa chama hicho wa kuteua jina la Mgombea Uspika kupitia CCM uliofanyika leo Jumatatu Novemba 16, 2015 katika makao makuu ya Chama hicho mjini Dodoma.
 Wabunge Watelue wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elibariki Kingu (Ikungi) (katikati), Khamis Gulamali (Manonga) kulia na Musa Ntimizi (Igalula) wakibadilishana mawazo mara baada ya kumalizika kwa mkutano maalum wa wabunge wa chama hicho wa kuteua jina la Mgombea Uspika kupitia CCM uliofanyika leo Jumatatu Novemba 16, 2015 katika makao makuu ya Chama hicho mjini Dodoma.
 Wabunge Wateule kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. George Mkuchika (Newala Mjini) (kulia)na Venance (Mwamoto Kilolo) wakibadilishana mawazo mara baada ya kumalizika kwa mkutano maalum wa wabunge wa chama hicho wa kuteua jina la Mgombea Uspika kupitia CCM uliofanyika leo Jumatatu Novemba 16, 2015 katika makao makuu ya Chama hicho mjini Dodoma.
 Mbunge wa Bunge wa Afrika Mashariki, Mhe. Abdullah Ali Mwinyi (kulia)akibadilishana mawazo na Mbunge mteule wa Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga mara baada ya kumalizika kwa mkutano maalum wa wabunge wa chama hicho wa kuteua jina la Mgombea Uspika kupitia CCM uliofanyika leo Jumatatu Novemba 16, 2015 katika makao makuu ya Chama hicho mjini Dodoma.PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO NA ADAM MZEE

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MKUTANO WA WABUNGE WA CCM WAMPITISHA MBUNGE WA KONGWA-CCM JOB NDUGAI KUWA MGOMBEA PEKEE WA NAFASI YA USPIKA
MKUTANO WA WABUNGE WA CCM WAMPITISHA MBUNGE WA KONGWA-CCM JOB NDUGAI KUWA MGOMBEA PEKEE WA NAFASI YA USPIKA
http://4.bp.blogspot.com/-ki0Qf57vodo/VknlW144JVI/AAAAAAADbDc/JP3QVu4RCp4/s640/2.jpg
http://4.bp.blogspot.com/-ki0Qf57vodo/VknlW144JVI/AAAAAAADbDc/JP3QVu4RCp4/s72-c/2.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/11/mkutano-wa-wabunge-wa-ccm-wampitisha.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/11/mkutano-wa-wabunge-wa-ccm-wampitisha.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago