Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

GAPCO KUDHAMINI KILIMANJARO MARATHON KILOMITA 10 KWA WALEMAVU 2016

Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa pili kutoka kushoto) akishiriki katika uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo...

Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa pili kutoka kushoto) akishiriki katika uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za kilomita 10 kwa walemavu. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania Oscar Shelukindo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli, Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni, Alex Nkenyenge na Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha.
Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (Wa tatu kutoka kushoto) akishiriki katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo GAPCO ilitangaza kudhamini mbio za kilomita 10 kwa walemavu. 

---
 GAPCO, kampuni ya mafuta inayoongoza Tanzania imetangaza udhamini wake wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016 kilomita 10 kwa walemavu. Akitangaza udhamini huo jana wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi alisema GAPCO inaona fahari kudhamini mbio hizo za kilomita 10 kwa walemavu. “Tumeshuhudia mbio hizi za Kilimanjaro Marathon zikikua tangu tuanze kudhamini mwaka 2011 na pia kufurahia faida wanayopata washiriki na jamii inayozunguka maeneo ambayo mbio hizi hufanyika kila mwaka.

 Tunayo furaha kufanya kazi na Wild Frontiers ambao ndio waandaaji wa mashindano haya,” alisema Kakwezi. “Kama sehemu ya kusaidia jamii ambayo tunafanya biashara, GAPCO Tanzania imeamua kusaidia wanariadha ambao ni walemavu kwa kudhamini mbio ambazo wanashiriki walemavu pekee,” alisema. Alisema udhamini wa GAPCO pia utahusisha usafiri, malazi na chakula kwa washiriki kutoka Dar es Salaam na pia zawadi za pesa kwa washindi wa mbio hizo za kilomita 10 ambazo zinafanyika pamoja na mbio nyingine za Kilimanjaro Marathon. Kakwezi aliendelea kusema kuwa Kilimanjaro Marathon limekua tukio kubwa linalovutia washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania na hivyo limesaidia sana kutangaza vivutio vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro na pia kuwaongezea kipato wafanyabiashara wa Moshi.”.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: GAPCO KUDHAMINI KILIMANJARO MARATHON KILOMITA 10 KWA WALEMAVU 2016
GAPCO KUDHAMINI KILIMANJARO MARATHON KILOMITA 10 KWA WALEMAVU 2016
http://3.bp.blogspot.com/-kslRG8v2fVY/VkzgGtF3XnI/AAAAAAABpQA/I7vcMYVaC0g/s640/IMG_2071.jpg
http://3.bp.blogspot.com/-kslRG8v2fVY/VkzgGtF3XnI/AAAAAAABpQA/I7vcMYVaC0g/s72-c/IMG_2071.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/11/gapco-kudhamini-kilimanjaro-marathon.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/11/gapco-kudhamini-kilimanjaro-marathon.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago