Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA :NAMALIZA UONGOZI KWA AMANI, FURAHA

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda ---   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  OFISI YA WAZIRI MKUU     *Asihi viongozi, watumishi wa umma ...

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda
---
 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
OFISI YA WAZIRI MKUU
 
 *Asihi viongozi, watumishi wa umma wasiache kumuomba Mungu
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kumaliza salama utumishi wake Serikalini kwenye ngazi za juu ambao umedumu kwa takriban miaka 15.

Akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki wakati wa Ibada ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Anna iliyoko Hananasifu, Kinondoni leo mchana (Jumapili, Oktoba 18, 2015), Waziri Mkuu Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na miezi tisa; pia katika ngazi ya uwaziri miaka miwili na nusu na miaka mitano akiwa Naibu Waziri.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumaliza uongozi wangu Serikalini. Ninamaliza uongozi wangu kwa amani na furaha. Katika ibada hii ya shukrani nimemuomba Mungu anisamehe kwa matamshi niliyoyatoa nikiwa kiongozi… yanaweza kuwa yaliwaudhi watu bila mimi kujua,” alisema.

“Uwaziri Mkuu ni kazi ngumu yenye changamoto nyingi. Nitakuwa mtu wa ajabu nisipomshukuru Mungu kwa uongozi wake katika kipindi chote hicho tangu nikiwa Naibu Waziri hadi kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu,” alisema.

“Wito wangu kwa Watanzania wote ni kwamba msiache kumtaguliza Mungu maishani kwa sababu yeye ndiye mtoaji wa yote. Wote tuendelee kumtii Mungu na viongozi wetu wa kiroho kwa sababu wako hapa kumwakilisha yeye,” alisema.

Alisema wako baadhi ya watu ambao wakipata madaraka wanaona kwenda kanisani ni kero au ni kupoteza muda. “Tatizo lao ni kutojijua, hawatambui kwamba bila Mungu hizo nafasi wasingezipata. Ninawaomba tujue kwamba kuna maisha hata nje ya utumishi wa umma na utumishi wa kisiasa,” alisema.

Alisema katika utumishi wake wa umma amejifunza mambo mengi lakini kikubwa alichobaini ni kujua jinsi ya kuishi na watu. “Elimu kubwa ni kujua jinsi ya kuishi, hii ni elimu zaidi ya kitabuni,” alisema. Alitumia fursa hiyo kumshukru mke wake, Mama Tunu Pinda kwa kuwa nguzo ya familia na kuwalea watoto wote walionao wakati yeye akihangaika na masuala ya kitaifa.

Katika hatua nyingine, Abate Thadei Mhagama kutoka Abasi ya Hanga iliyoko Songea ambaye aliongoza ibada hiyo, aliwataka waumini wote nchini wazidishe sala kwa kufunga na kuomba katika siku saba zilizobakia kabla ya uchaguzi mkuu kwa sababu hali ni tete.

“Ninawaomba waumini wote tuzidishe sala ili kwanza pawe na amani na upendo na pia Mungu atuwezeshe kupata viongozi aliowandaa kwa maana ya Rais, Wabunge na Madiwani.”
“Sote ni mashahidi, tumeona kwenye mikutano kila mgombea akija sote tunajaa huko… hii ni kwa sababu hatujuia yupi ni yupi, ndiyo maana nasisistiza kuwa tumuombe Mungu atuletee yule ambaye amemuandaa,” aliongeza.

Alisema kila mwananchi amesikia kwamba uchaguzi ukishafanyika awe tayari kupokea matokeo. “Tumeambiwa mara kadhaa tuwe tayari kukubali matokeo… kwa vile tunamuomba Mungu kwa bidii, itakuwa rahisi kukubali hayo matokeo kuliko kwa wale ambao wanaenda bila kuongozwa na Mungu,” alisema.

“Litakuwa jambo jepesi kwetu kukubali matokeo kwani tutasema Mungu amemleta yule aliyemuandaa, yule ambaye tumekuwa tukimuomba atuletee,” alisisitiza.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza la Walei la Parokia hiyo, Bw. Arbogasti Warioba alisema kama kanisa wao wanamshukuru Mungu kwa ulinzi aliompatia Mhe. Pinda kwa kipindi chake chote cha Uwaziri Mkuu.

“Sote tunatambua kuwa kazi ilikuwa ngumu, misafara ilikuwa ni mingi na wakati mwingine ya mwendo mkali lakini Mungu alikutetea na kukulinda hadi leo uko salama. Tunakushukuru pia kwa ushirikiano ulioendelea kutuonyesha wakati ukiwa madarakani na tunakuombea uendelee kuwa na uchaji wa Mungu katika maisha yako ya uraiani,” alisema Bw. Warioba.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI, 
S.L. P. 3021,
11410 
DAR ES SALAAM
JUMAPILI, OKTOBA 18, 2015.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA :NAMALIZA UONGOZI KWA AMANI, FURAHA
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA :NAMALIZA UONGOZI KWA AMANI, FURAHA
http://1.bp.blogspot.com/-n7zu8a5evLA/ViUC9S_5ylI/AAAAAAADZyY/uQiz7EZE8lA/s640/IMG_0007.JPG
http://1.bp.blogspot.com/-n7zu8a5evLA/ViUC9S_5ylI/AAAAAAADZyY/uQiz7EZE8lA/s72-c/IMG_0007.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/10/waziri-mkuu-mizengo-pinda-namaliza.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/10/waziri-mkuu-mizengo-pinda-namaliza.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago