Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Y. Senkondo (kulia) akifafanua jambo kwa Waandishi...

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa
Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Y. Senkondo (kulia) akifafanua
jambo kwa Waandishi wa Habari namna ofisi yake inavyoratibu uendeshaji
wa mikutano kwa njia ya video (Video Conference). Kushoto ni Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. Florence
Temba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa
Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Y. Senkondo (kulia),
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais – Utumishi Bw.
Florence Temba (katikati) na Mratibu wa Mafunzo wa TaGLA Bw. Dickson
Mwanyika (kushoto) wakishiriki mkutano kwa njia ya video (Video
Conference) uliofanyika kwa kushirikiana na Kenya School of Government.
Wengine ni Waandishi wa Habari kutoka katika Vyombo mbalimbali vya
habari nchin.
---
Na Anitha Jonas – MAELEZO. Dar es Salaam.
Serikali imewasihi watanzania
kutumia huduma ya mafunzo kwa njia ya mtandao kwani inapunguza gharama
na kurahisisha upatikanaji wa majibu ya haraka.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi
Mtendaji,Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao(TaGLaA) Bw.Charles
Senkondo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 19, 2015
jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo pamoja na
kuanzishwa kwa maktaba ya kisasa za maendeleo ikishirikiana na wadau
mbali mbali ndani na nje ya nchi.
“Wakala imefanikiwa kushirikiana
na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kutumia mitandao ya
kiteknolojia na imeweza kufundisha mfumo wa malipo ya mishahara kwa
watumishi wa serikalini watendaji wakuu kutoka taasisi za serikali,
wakurugenzi wa halmashauri za wilaya pamoja na wakurugenzi wa
rasilimali watu wapatao 1,200,”alisema Bw.Senkondo.
Hata hivyo Bw.Senkondo alisema
gharama za kutumia huduma hizi za mafunzo ya mtandao kupitia video ni
shillingi 400,000/= kwa saa moja na mikutano hii inaweza kufanyika hata
kwa kuwaunganisha watu wa mikoani moja kwa moja na nchi za kimataifa.
Mkurugenzi huyo aliendelea
kusema wakala imefanikiwa kuendesha kesi za mahakama kwa kutumia huduma
ya mahojiano ya video kwa watu kuweza kutoa ushahidi kwa njia ya video
na kusaidia kupunguza gharama pamoja na huhamasiha maamuzi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo
alieleza changamoto mbalimbali zinazoikumba taasisi hiyo ikiwemo ufinyu
wa nafasi za ofisi na kufafanua kuwa kuna jitihada za kupata eneo la
kujenga ofisi zitakazo kidhi mahitaji ya wakala.
Jumla ya washiriki 20,322
wamepata mafunzo kutokana na midahalo iliyofanyika pamoja na mafunzo 783
ya kubadilishana maarifa yaliyoendeshwa kupitia wakala katika kipindi
cha mwaka 2005 mpaka 2015.