Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MKURUGENZI WA MAKAMPUNI YA APEX GROUP AOMBA WANANCHI KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU KATIKA UCHAGUZI MKUU UTAKAO FANYIKA KESHO KUTWA KOTE NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Apex Group na Mwanaharakati,  Joseph Mhonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa haba...Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Apex Group na Mwanaharakati,  Joseph Mhonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho nchini kote. Kulia ni Ofisa Habari wa Makampuni hayo, Pipino Sudi.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara Habari Maelezo, Vicent Tiganya (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Ofisa Habari wa Makampuni hayo, Pipino Sudi na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Apex Group na Mwanaharakati,  Joseph Mhonda.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mkuu wa Makampuni ya Apex Group na Mwanaharakati, Joseph Mhonda amewataka wananchi kupiga kura kwa amani ili kulinda amani iliyopo nchini hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini kote kesho kutwa.

Akizungumza Dar es Salaam leo  Mkurugenzi huyo alisema amani ya nchi inapaswa kuzingatiwa katika kipindi hiki cha siku ya kupiga kura , siku ya kutangazwa washindi na siku ya kusubiria majibu ya mshindi.

"Siku hizi tatu ni ngumu sana lakini ni vyema wananchi wakawa makini katika kulinda amani na upendo wa nchi yetu kwani hii ndiyo nguzo kubwa katika kipindi hiki," alisema.

Mhonda pia alizungumza kuwa katika kutangazwa matokeo hayo pia ni vyema matokeo hayo wananchi kuyakubali kwa moyo mmoja kwani kutokubali matokeo kunaweza kuleta mkanganyiko wa amani.

Alisema amani ya nchi ikilindwa itakuwa ni vyema hasa katika masuala ya kuleta maenedeleo ya nchi hasa ukizingatia kuwa nchi inaenda kutafuta maendeleo.

Akizungumzia suala la kulinda kura Mhonda alisema  kila chama kinatakiwa kuwaamini mawakala ambao wamewaweka katika vituo na si kutaka kulinda  nje.

"Watu wanaosema kuwa kura zinatakiwa kulindwa watakuwa hawawaamini wale mawakala ambao wanaweka katika vituo vya kuwapiga kura ili kusimamia kura zao,"alisema.

Akizungumzia suala la mita 200 alisema hiyo ni sheria ambayo ipo katika tume ya uchaguzi  hivyo haina budi kutekelezwa.

Mhonda alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuchagua kiongozi bora ambaye atakuwa mstari wa mbele kupigania maendeleo ya wananchi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MKURUGENZI WA MAKAMPUNI YA APEX GROUP AOMBA WANANCHI KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU KATIKA UCHAGUZI MKUU UTAKAO FANYIKA KESHO KUTWA KOTE NCHINI
MKURUGENZI WA MAKAMPUNI YA APEX GROUP AOMBA WANANCHI KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU KATIKA UCHAGUZI MKUU UTAKAO FANYIKA KESHO KUTWA KOTE NCHINI
http://1.bp.blogspot.com/--GUuhcePHFU/ViooCLpPslI/AAAAAAAAT4E/pZU9-vgeiPs/s640/1.JPG
http://1.bp.blogspot.com/--GUuhcePHFU/ViooCLpPslI/AAAAAAAAT4E/pZU9-vgeiPs/s72-c/1.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/10/mkurugenzi-wa-makampuni-ya-apex-group.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/10/mkurugenzi-wa-makampuni-ya-apex-group.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago