Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MAZISHI YA MWENYEKITI MWENZA UKAWA DK.EMMANUEL MAKAIDI KUFANYIKA MAKABURI YA SINZA, MWILI WAKE KUAGWA KESHO ASUBUHI VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM

Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela Makaidi akiwa katika h...

Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela Makaidi akiwa katika huzuni baada ya kuondokewa na mpendwa wake.
Mtoto wa kwanza wa Dk. Makaidi, Hilda Emmanuel Makaidi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
Mtoto wa marehemu Mhandisi Emmanueli Makaidi (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ratiba ya mazishi ya baba yake.
Ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa Dk.Makaidi Sinza.
Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela Makaidi (kulia), akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwake Sinza Vertican Dar es Salaam kesho asubuhi.
--
Na Dotto Mwaibale

MWILI wa Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Dk. Emmanueli Makaidi unatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, mtoto wa marehemu Mhandisi Emmanueli Makaidi alisema mwili huo baada ya kutoka Masasi ulipelekwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na leo jioni utapelekwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza Vertican ambapo itafanyika ibada fupi na kupata fursa ya ndugu na majirani kuuaga.

Alisema kesho mwili huo utaagwa katika viwanja vya Karimjee ambapo viongozi mbalimbali wa kisiasa, serikali watakuwepo na kisha kufanyika mazishi yake katika makaburi ya Sinza. 


"Unajua baba alikuwa ni mwanasiasa na amefariki akiwa bado ni mwanasiasa hivyo ni lazima uweze kuagwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali" alisema.

Akimzungumzia baba yake alisema marehemu alikuwa ni mtu ambaye anapenda utu ambapo alipenda kila binadamu ni sawa na hapaswi kubaguliwa.

Alisema wameamaua kumzika baba yao Dar es Salaam na si Mtwara kutokana na mke na mama yake kuzikwa Dar es Salaamna ndio utaratibu waliouweka wa kuzikwa.

"Baba alitaka kila mtu ambaye atafariki ni vyema akazikiwa hapo kwani hata wakati wa kulimia makaburi inakuwa rahisi,"alisema.

Kwa upande wake mtoto wa pili wa Marehemu Hilda Makaidi alisema baba yao alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu.

"Nakumbuka nilimpigia baba simu akiniambia mwanangu Hilda Masasi kugumu, na mimi nikamwambia baba rudi nyumbani tukutibu lakini hakukubali haraka,"alisema.

Alisema baba ameacha mjane na watoto 10 huku ikiwa wakike wakiwa wanne na wakiume sita na wajukuu 10 na vitukuu sita.

Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi George Kahangwa alisema mazishi hayo yatahuduliwa na mgombea urais wa umoja huo Edward Lowassa  pamoja na viongozi wa taifa wa serikali na vyama vya siasa na vyama vya michezo.

"Sote tushiriki kumpa heshima za mwisho na kumsindikiza mpendwa wetu katika safari ya mwisho,"alisema. 

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MAZISHI YA MWENYEKITI MWENZA UKAWA DK.EMMANUEL MAKAIDI KUFANYIKA MAKABURI YA SINZA, MWILI WAKE KUAGWA KESHO ASUBUHI VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM
MAZISHI YA MWENYEKITI MWENZA UKAWA DK.EMMANUEL MAKAIDI KUFANYIKA MAKABURI YA SINZA, MWILI WAKE KUAGWA KESHO ASUBUHI VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM
http://2.bp.blogspot.com/-ctptDUk6O7o/ViTz77YOzwI/AAAAAAAATxY/N78Jf9H3ZbM/s640/1.JPG
http://2.bp.blogspot.com/-ctptDUk6O7o/ViTz77YOzwI/AAAAAAAATxY/N78Jf9H3ZbM/s72-c/1.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/10/mazishi-ya-mwenyekiti-mwenza-ukawa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/10/mazishi-ya-mwenyekiti-mwenza-ukawa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago