Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LATOA MSIMAMO WAKE JUU YA SUALA LA MITA 200 BAADA YA KUPIGA KURA.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake ...


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana ambapo alitoa msimamo wa jeshi hilo juu ya suala la wananchi kubaki mita 200 kutoka vilipo vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura siku ya jumapili Octoba 25,2015 ikiwa ni siku ambayo Watanzania watashiriki katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Kuwachagua Wawakilishi wao kuanzia ngazi ya Madiwani, Wabunge na Rais.
--
Kamanda Mkumbo alisema kuwa jeshi la polisi linawataka wananchi wote kurejea majumbani mwao baada ya kupiga kura badala ya kubaki mita 200 kutoka vilipo vituo vya kupigia kura kama ambavyo baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa wamekuwa wakiwashauri kwa ajili ya kulinda kura.

Alisema Jeshi hilo linapiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote siku hiyo ya uchaguzi na kwamba litawachukulia hatua kali wale wote watakaoonekana kwenda kinyume na agizo hilo ikiwa ni pamoja na kuvaa sare za vyama vya siasa ama kuonyesha ishara zozote za vya hivyo.

Wakati huo huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP.Ernest Mangu nae ametoa tamko kama hilo akiwataka watanzania kurejea majumbani baada ya zoezi la kupiga kura akisema kuwa jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa linaimarisha usalama kwa wananchi watakaokuwa wakitoka majumbani kwenda kupiga kura na kurejea majumbani mwao.

Hata hivyo Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es salaam hii leo inatarajia kutoa maamuzi yake juu ya suala hilo la uhalali wa wananchi kubaki umbali wa mita 200 kutoka vilipo vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo
Mwanahabari
Wanahabari

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LATOA MSIMAMO WAKE JUU YA SUALA LA MITA 200 BAADA YA KUPIGA KURA.
JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LATOA MSIMAMO WAKE JUU YA SUALA LA MITA 200 BAADA YA KUPIGA KURA.
http://1.bp.blogspot.com/-XmlEFrLyqSU/Vim-gNfm99I/AAAAAAAAHSA/XiW7utPzd4w/s640/1.JPG
http://1.bp.blogspot.com/-XmlEFrLyqSU/Vim-gNfm99I/AAAAAAAAHSA/XiW7utPzd4w/s72-c/1.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/10/jeshi-la-polisi-mkoani-mwanza-latoa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/10/jeshi-la-polisi-mkoani-mwanza-latoa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago