Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

JESHI LA POLISI MBEYA LAPIGA MARUFUKU KWENDA KUPIGA KURA UKIWA UMEVAA SARE ZA VYAMA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ----- Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limetoa rai kwa wafuasi wa vyama vishiriki katika uchaguzi mku...


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
-----
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limetoa rai kwa wafuasi wa vyama vishiriki katika uchaguzi mkuu Octoba 25 mwaka huu kujiepusha kufika katika kituo cha kupigia kura wakiwa wamevaa nguo zenye picha za wagombea, maneno au nembo ama rangi za chama cha siasa.


Aidha wametakiwa , kuepuka kutumia uvumi, maneno ya uongo, hisia au visingizio vyenye lengo la kuwazuia wengine kwenda kupiga kura.

Pia amewataka  kuepuka kufanya kampeni katika kituo cha kupigia kura iwe kwa maneno ya ushawishi au kwa kuonyesha ishara ya chama fulani cha siasa.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ahmed Msangi amesema nivema kila mwananchi anae stahili kupiga kura ahakikishe anafuata taratibu hizo ili kujiepusha na vitendo vya uvujifu wa amani katika siku hiyo muhimu.


Amesema  vyema kila mwananchi kupiga kura kwa kutumia jina na kitambulisho chake na sio cha mtu mwingine, aliyekufa au mgonjwa, kuepuka kufanya fujo ama vurugu katika kituo cha kupigia kura.


Aidha amesisitiza kuwa   kila mpiga kura mara baada ya kupiga kura kuondoka kwenye kituo cha kupigia kura na kuendelea na shughuli nyingine kwani ni kosa kupiga kura na kuendelea kubaki katika eneo la kituo cha kupigia kura.


Amesema  ni wajibu wa jeshi la polisi kuwalinda maofisa wanaosimamia uchaguzi, kuhakikisha kwamba zoezi la upigaji kura linaenda sawa, bila vikwazo au bughudha na kuhakikisha vifaa vya kupigia kura viko salama.


Kwa mkoa wa mbeya tuna jumla ya majimbo 13 ya uchaguzi, vituo 3,899 vya kupigia kura, kila kituo kitalindwa na askari ili kuhakikisha suala la ulinzi na usalama linaimarishwa kwa kipindi chote cha zoezi la kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi.


Msangi amesema Jeshi la polisi mkoa wa mbeya limejipanga kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ikiwa ni pamoja na vituo vya kupigia kura sanjali na kuwepo kwa  na doria za magari, pikipiki, mbwa na askari ambao watakuwa wakitembea huku na kule kwa lengo la kudhibiti vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani.

JAMIIMOJABLOGCOMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: JESHI LA POLISI MBEYA LAPIGA MARUFUKU KWENDA KUPIGA KURA UKIWA UMEVAA SARE ZA VYAMA
JESHI LA POLISI MBEYA LAPIGA MARUFUKU KWENDA KUPIGA KURA UKIWA UMEVAA SARE ZA VYAMA
http://1.bp.blogspot.com/-1wYeag0R04M/VioimzpbedI/AAAAAAAAUbQ/JwYPZeqfiS0/s640/MSANGI.JPG
http://1.bp.blogspot.com/-1wYeag0R04M/VioimzpbedI/AAAAAAAAUbQ/JwYPZeqfiS0/s72-c/MSANGI.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/10/jeshi-la-polisi-mbeya-lapiga-marufuku.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/10/jeshi-la-polisi-mbeya-lapiga-marufuku.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago