Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WATANO WAFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO TOFAUTI MKOANI MBEYA WAMO RAIA WA ETHIOPIA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi. -----      Na Jamiimojablog.        Watu watano wamefariki dunia     Mkoan...


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
-----

     Na Jamiimojablog.

       Watu watano wamefariki dunia   Mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti likiwemo la ajali ya haice iliyosababisha vifo vya watu wanne mkoani hapa.
       
         Katika tukio la kwanza gari  lenye namba za usajili  T.519 Akh aina ya Toyota Haice ikiendeshwa na dereva  asiyefahamika kugongana na pikipiki yenye namba za usajili  T.535 Awc aina Ya T-Better eneo la Nanenane Jijini Mbeya.

      Ajali hiyo imetokea Septemba  29 majira ya  Saa 4 usiku katika eneo la   Nane-Nane, Kata Ya Isyesye,  barabara Kuu ya Mbeya/Njombe .

        Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amewataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa mwendesha  pikipiki ambaye bado jina lake halijafahamika sanjali na wengine watatu raia wa Ethiopia ambao majina yao bado hayajafahamika mara moja  ambao walikuwa  wamepakizwa kwa pamoja kwenye pikipiki hiyo kwa mtindo maarufu wa Mshikaki.

       Aidha Katika ajali hiyo  Edward Aloyce (42) Mkazi Wa Uyole ambaye alikuwa abiria kwenye  Haice alijeruhiwa na amelazwa katika   Hospitali ya Rufaa Mbeya. 

          Kwa mujibu  wa  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Msangi  amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo ya abiria pamoja na pikipiki hiyo.

       Amesema  dereva wa hiace alikimbia mara baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo jitihada za kumsaka zikiendelea kufanyika na jeshi hilo miili ya  marehemu imehifadhiwa  Hospitali Ya Rufaa Mbeya.

        Katika tukio jingine mtu mmoja  Mkazi wa  Masoko Wilaya ya Rungwe  Ndugu  Tukupyelesya Enock Mwakifuna (54) amefariki dunia mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria  T.913 Amb aina Ya Toyota Hillux ikiendeshwa na dereva asiyefahamika  kuacha njia na kupinduka  huko katika kijiji cha  Masoko,  Wilaya Ya Rungwe, Mkoa Wa Mbeya bararabara ya Tukuyu/Lwangwa.

      Aidha Katika ajali hiyo abiria Watatu wanawake wawili na Na mwanaume mmoja walijeruhiwa na wamelazw katika hospital ya  Hospitali ya Wilaya Rungwe huku chanzo cha . ajali hiyo ni mwendo kasi  dereva .

     Kufuatia matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Ahmed Msangi ametoa o wiito  Kwa madereva kuwa  Makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza Kuepukika.
 mwisho

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WATANO WAFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO TOFAUTI MKOANI MBEYA WAMO RAIA WA ETHIOPIA
WATANO WAFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO TOFAUTI MKOANI MBEYA WAMO RAIA WA ETHIOPIA
http://2.bp.blogspot.com/-k0bbj8RgXN0/VgvC_awTsWI/AAAAAAAAUCo/Mqst4xMyYy4/s640/MSANGI.JPG
http://2.bp.blogspot.com/-k0bbj8RgXN0/VgvC_awTsWI/AAAAAAAAUCo/Mqst4xMyYy4/s72-c/MSANGI.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/09/watano-wafariki-dunia-katika-matukio.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/09/watano-wafariki-dunia-katika-matukio.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago