Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WAHINDU WAADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA MUNGU WAO MDOGO MWENYE DARAJA KUBWA WAMUWEKA BAHARINI JIJINI DAR ES SALAAM

  Mungu huyo wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa anayejulikana kwa zaidi ya majina 125 (Ganpati Bappa Morya)  mwenye sura ya tembo ak...


 Mungu huyo wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa anayejulikana kwa zaidi ya majina 125 (Ganpati Bappa Morya)  mwenye sura ya tembo akiwa amewekwa juu ya gari maalumu wakipita mitaa kadhaa ya jiji la Dar es Salaam leo mchana akipelekwa Baharini ili kuungana na mungu wa kike waliopo kwenye mito mitatu mikubwa mitakatifu iliyopo nchini India.
 Mungu huyo akiwa amewekwa juu ya paa la gari akiwa katika uangalizi wa heshima.
 Wanawake wa madhehebu hayo ya kihindu wakicheza wakati wa kuadhimisho siku hiyo.
 Hapa ni furaha tupu ya maadhimisho hayo.
 Hapa wazazi na watoto wakiwa kwenye maandamano hayo kuelekea baharini kumuweka ili kuungana na mungu wengine wa kike waliopo katika mito mitatu mitakatifu iliyopo nchini India.
 Maandamano yakiendelea.
Hapa ni furaha tupu kwa wanawake, wanaume, wazee na watoto.
 Watoto wakifurahia maadhimisho hayo.
 Hapa wakiwa juu ya magari kuelekea kumsindikiza mungu wao huyo.
 Hapa wakiwa kwenye magari kuelekea baharini.
 Ni furaha tupu ndani ya gari.
Safari ya kwenda baharini ikiendelea.
--
Na Dotto Mwaibale

WATANZANIA wenye asili ya India wa dhehebu la Hindu (Baniani), leo wameadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mungu wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa (Ganpati Bappa Morya) na mwenye sura ya tembo.

Mungu huyo hufanyiwa sherehe baada ya kufanyika kwa ibada ya siku tisa ambapo siku yake ya kuzaliwa alipelekwa baharini kwaajili ya kuungana na Mungu wa kike walio kwenye mito mitatu mitakatifu iliyopo nchini India ambayo ni Sarasgad, Amba na Raigad.

Sherehe hizo zilianza kwa ibada ambapo pia walitumia fursa hiyo kuiombea amani ya nchi hii katika maadhimisho ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa iliambatana na utoaji wa sadaka za vyakula mbalimbali na maombi hupelekwa baharini kwa ajili ya kuungana na Mungu kike.

Katika sherehe hizo jijini hapa zilianzia katika nyumba zao za ibada ambapo kulikuwa na msafara mkubwa ambao ulihusisha na magari yaliyobeba Mungu huyo huku wanawake wakijipamba kwa mavazi mazuri huku wakitembea na kucheza kwa furaha kumsindikiza wakipita barabara kadhaa za katikati ya jiji la Dar es Salaam zikiwemo za Azikiwe na Kivukoni hadi Baharini.

Baada ya kufanyika kwa sherehe hizo pia baada ya miezi miwili kutakuwa na maadhimisho ya mwaka mpya ambao ni Diwali ambapo mwaka ujao wataadhimisha tena sherehe hizo.

Mungu huyo ambaye pia hujulikana kwa majina zaidi ya 125 na ndiye Mungu mdogo na mwenye daraja kubwa zaidi.Baadhi ya majina hayo ni Ganesh Chaturthi, Vinayaka Chaturthi

Inaaminika kuwa unapoomba kitu chochote kutoka kwake unafanikiwa. Ambapo mungu huyo ambaye ni mwanaume aliyetengenezwa kwa aina ya udongo maalumu huyeyuka anapowekwa baharini ikiwa na maana ya kwenda kuungana na Mungu wa kike waliokatika mito hiyo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WAHINDU WAADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA MUNGU WAO MDOGO MWENYE DARAJA KUBWA WAMUWEKA BAHARINI JIJINI DAR ES SALAAM
WAHINDU WAADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA MUNGU WAO MDOGO MWENYE DARAJA KUBWA WAMUWEKA BAHARINI JIJINI DAR ES SALAAM
http://3.bp.blogspot.com/-yP5D8zgtDKc/Vgf0-vD8NfI/AAAAAAAATW4/T0XEUXbfBys/s640/1.JPG
http://3.bp.blogspot.com/-yP5D8zgtDKc/Vgf0-vD8NfI/AAAAAAAATW4/T0XEUXbfBys/s72-c/1.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/09/wahindu-waadhimisha-siku-ya-kuzaliwa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/09/wahindu-waadhimisha-siku-ya-kuzaliwa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago