Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

UMEME WA PUMBA ZA MCHELE, MASHUDU YA PAMBA WATUMIKA KUENDESHEA MITAMBO YA TBL MWANZA

 Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mwanza, Raymond Richmond,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni hiyo ...


 Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mwanza, Raymond Richmond,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni hiyo  kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba,kama chanzo cha nishati ya umeme kinachotumika kuendeshea mitambo.Kushoto ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi.
Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond, akizungumzia mradi wa matumizi ya mapumba ya mchele na mashudu ya pamba,ambacho ni chanzo cha nishati ya kuendesha mitambo kiwandani hapo.Nishati ni rafiki wa mazingira  kwa sababu haina hewa ukaa.Wanaokoa Dola za Kimarekani (USD) 400,000 hadi 500,000 kwa mwaka ambazo zingetumika kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendeshea mitambo .
Waandishi wa habari wakiongozwa na  Meneja wa Kiwanda cha kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond(wa kwanza kushoto), kwenda kutembelea mtambo unaotumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba kuzalisha nishati ya umeme inyotumika kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa TBL, Sunday Kidolezi.
Meneja wa Nishati na Maji wa Kampuni ya Bia (TBL)Mwanza, Sunday Kidolezi (wa kwanza kulia),wakiwa na waandishi wa habari wakati wakitembelea mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.wa Kwanza kutoka kushoto (mwenye shati jeupe), Ni Meneja wa Kiwanda hicho, Raymond Richmond.
Meneja wa Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,Raymond Richmond (mwenye shati jeupe) akiwaonesha waandishi wa habari mtambo unaozalisha nishati ya umeme kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.anaoshuhudia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo,Sunday Kidolezi (mwenye fulana ya mistari).Mwingine ni mwandishi wa habari wa kampuni ya The Guardian, Daniel Mkate,ambaye ni miongoni mwa  waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho.
Raymond Richmond, Meneja wa kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), mapumba ya mchele,yanayotumika kuzalisha nishati ya umeme wa kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo.
Mwandishi wa habari, Daniel Mkate (kushoto) akiwauliza maswali, Meneja wa  Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond na Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi, kuhusu  changamoto ya upatikanaji wa mali ghafi hiyo na madhara yake katika kuzalisha nishati na athari za mazingira.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni ya Bi (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba kwenye magunia, kabla ya kuingizwa kwenye mtambo wa kuzalisha umeme kiwandani hapo.Hapo ni katika eneo  linalotumika kupakulia shehena ya mapumba hayo ya mchele, kutoka kwa msambazaji.
Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,Raymond Richmod, akiwaonyesha waandishi wa habari, Daniel Mkate wa TRhe Guardian (nyuma) na Henry Kavirondo wa Chanel Ten,mashine inayosukuma mapumba ya mchele na mashudu ya pamba, kwenda kwenye mtambo wa kufua umeme unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba ya mchele kwenye mashine kwa ajili ya kuyasukuma kadi kwenye mtambo wa kuzalisha nishati ya umeme, unaotumiwa kuendesha mitambo ya uzalishaji ya kiwanda hicho.
Meneja wa Maji na Nishati wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Sunday Kidolezi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhudu mradi huo wa uzalishaji wa nishati ya umeme,unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda cha kampuni hiyo kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.Wa kwanza kushoto ni Meneja wa kiwanda cha kampuni hiyo,Raymond Richmond.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: UMEME WA PUMBA ZA MCHELE, MASHUDU YA PAMBA WATUMIKA KUENDESHEA MITAMBO YA TBL MWANZA
UMEME WA PUMBA ZA MCHELE, MASHUDU YA PAMBA WATUMIKA KUENDESHEA MITAMBO YA TBL MWANZA
http://1.bp.blogspot.com/-M01ERJlGwMI/Ve8qGHkmbSI/AAAAAAAA5UU/rc02J3cmW7A/s640/TBL%2B1.jpg
http://1.bp.blogspot.com/-M01ERJlGwMI/Ve8qGHkmbSI/AAAAAAAA5UU/rc02J3cmW7A/s72-c/TBL%2B1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/09/umeme-wa-pumba-za-mchele-mashudu-ya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/09/umeme-wa-pumba-za-mchele-mashudu-ya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago