Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

SOMA TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KUHUSU UZUSHI WA AFYA YA MKUU WA MAJESHI

  Jenerali Mwamunyange mara baada ya kuwasili na kupokelewa na mwenyeji wake Rome, nchini Italia. Jenerali Mwamunyange akikagua ...


 Jenerali Mwamunyange mara baada ya kuwasili na kupokelewa na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.
Jenerali Mwamunyange akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rome, nchini Italia
Jenerali Mwamunyange akiteta jambo na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.
KUMEKUWAPO UVUMI WENYE KUUPOTOSHA UMMA KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NCHINI AMENUSURIKA KIFO BAADA YA KUWEKEWA SUMU KATIKA CHAKULA NA HIVI SASA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN ILIYOPO NAIROBI, NCHINI KENYA, HUKU WENGINE WAKIDAI KUWA YUKO NCHINI INDIA KWA MATIBABU. 
TAARIFA HIZO NI UONGO WENYE KILA DALILI YA KUTENGENEZWA KWA LENGO LA KUWATIA HOFU WATANZANIA JUU YA USALAMA WA KIONGOZI HUYU WA JUU WA MAJESHI YETU.
UKWELI NI KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI, JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE NI BUKHERI WA AFYA NA HAYUPO NCHINI KENYA WALA INDIA KAMA ILIVYOENEZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA VYOMBO VYA HABARI.
TUNAPENDA KUWATOA HOFU WANANCHI KUWA TAARIFA HIZO NI UZUSHI MTUPU KWANI JENERALI MWAMUNYANGE ALIONDOKA NCHINI TAREHE 22 SEPTEMBA 2015, SAA 10.45 JIONI KWA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA EMIRATES KUELEKEA ROME, ITALIA KWA ZIARA YA KIKAZI KUFUATIA MWALIKO WA MKUU WA MAJESHI WA JAMHURI YA ITALIA, JENERALI CLAUDIO GRAZIANO. TUNAPENDA KUWAHAKIKISHIA WANANCHI KUWA JENERALI MWAMUNYANGE PAMOJA NA UJUMBE WAKE WANAENDELEA NA ZIARA HIYO KAMA ILIVYOPANGWA NA AMESIKITISHWA NA UVUMI HUO. 

WIZARA YA ULINZI YA JESHI LA KUJENGA TAIFA IMESIKITISHWA NA TABIA HII YA UZUSHI INAYOPINGANA NA WELEDI NA KANUNI ZA UANDISHI KATIKA TASNIA YA HABARI. NI DHAHIRI TABIA HII INAIDHALILISHA TASNIA YA HABARI NA WANAHABARI WANAOZINGATIA WELEDI NCHINI. TUNAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUKEMEA TAARIFA ZA AINA HII ZISIZOKUWA NA TIJA KWA TAIFA LETU NA ZILIZOLENGA KUWASUMBUA NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA WATUMISHI WENYE MAPENZI YA DHATI NA JENERALI MWAMUNYANGE.

TUNAWAASA WANAHABARI KUTOZITUMIA VIBAYA KALAMU ZAO NA UHURU WALIONAO KWA NAMNA YOYOTE ISIYOKUWA NA TIJA KWA TAIFA LETU. AIDHA, WIZARA NA TAASISI ZAKE WAKATI WOTE ZIMEKUWA TAYARI KUTHIBITISHA JAMBO LOLOTE AU KUTOA UFAFANUZI PALE ULIPOHITAJIKA. INASTAAJABISHA KUONA WALIOANZISHA UZUSHI HUO NA KUUENEZA HAWAKUWA TAYARI KUOMBA UTHIBITISHO WA NAMNA YOYOTE. JAMBO HILI LINATIA SHAKA JUU YA NIA YA MTU AU KIKUNDI KILICHOANZISHA UVUMI HUO.
WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA TAASISI ZAKE ZITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO WA DHATI KWA WANAHABARI WENYE NIA YA DHATI YA KUJENGA NA KUILETEA SIFA TASNIA YA HABARI KWA KUZINGATIA WELEDI. UHURU WA VYOMBO VYA HABARI UWE NI UHURU WENYE KUZINGATIA WAJIBU ULIOBAINISHWA KATIKA MAADILI NA KANUNI ZA UANDISHI WA HABARI.

MWISHO, TUNAWATAKA WALIOANZISHA UZUSHI HUO KUMUOMBA RADHI JENERALI MWAMUNYANGE KAMA ISHARA YA USTAARABU NA KUTAMBUA KUTELEZA KWAO. KUTOFANYA HIVYO ITATAFSIRIKA KUWA NI KUKIRI KUWA KUENEZA UZUSHI HUO HAIKUWA KUTELEZA, BALI ILIKUSUDIWA KWA DHAMIRA FULANI, NA HIVYO KUSHAWISHI HATUA ZAIDI KUCHUKULIWA.

JESHI NA WIZARA ZITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA HUSIKA KUWABAINI WATU WALIOHUSIKA KUUTUMIA VIBAYA UHURU WA HABARI NA HIVYO KUUPOTOSHA UMMA NA KULETA USUMBUFU KWA FAMILIA YA JENERALI MWAMUNYANGE, JESHI NA TAIFA KWA UJUMLA.
Imetolewa na
 Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
September 26, 2015.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: SOMA TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KUHUSU UZUSHI WA AFYA YA MKUU WA MAJESHI
SOMA TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KUHUSU UZUSHI WA AFYA YA MKUU WA MAJESHI
http://2.bp.blogspot.com/-eAWHwvhKWyc/VgfbYAkPKJI/AAAAAAADY7c/1QajNKCuTa8/s640/New-Picture-13-769x1024.png
http://2.bp.blogspot.com/-eAWHwvhKWyc/VgfbYAkPKJI/AAAAAAADY7c/1QajNKCuTa8/s72-c/New-Picture-13-769x1024.png
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2015/09/soma-taarifa-kwa-umma-kutoka-wizara-ya_27.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2015/09/soma-taarifa-kwa-umma-kutoka-wizara-ya_27.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago